Mgombea Urais CHADEMA Kupatikana Ndani ya Saa 72

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinaingia siku tatu ngumu za mchakato wa kupata mgombea urais wa Tanzania na Zanzibar katika uchaguzi mkuu utakaofanyika  Oktoba 28, 2020.

 

Chadema kitaanza mikutano yake kesho Jumapili tarehe 2-4 Agosti, 2020, katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

 

Pia kitatumia mikutano hiyo, kuwapata wagombea ubunge, wawakilishi na madiwani wa viti maalum na wabunge wa viti maalum.

 

Kesho Jumapili, itakuwa ni kikao cha Kamati Kuu ya Chadema, na Agosti 3 ni  zamu ya Baraza Kuu na mwisho Agosti 4 itakuwa ni mkutano mkuu.

 

Awali, mikutano hiyo ilipangwa kufanyika kati ya tarehe 27 hadi 29 Julai 2020, lakini ikasogezwa mbele kutokana na kifo cha rais wa awamu ya tatu,  Benjamin Mkapa.

Toa comment