The House of Favourite Newspapers

Mgombea wa Uenyekiti Simba Ajiondoa

ALIYEKUWA mgombe wa nafasi ya Uenyekiti katika klabu ya Simba ambaye pia ni nyota wa zamani wa timu hiyo, Mtemi Ramadhani, amejiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho leo ikiwa ni siku 9 pekee zimebaki kabla ya tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi huo ambao umepangwa kufanyika Novemba 3, 2018.
Mtemi ameweka wazi sababu zilizomfanya aondoe jina lake katika uchaguzi huo kwa kile alichodai kuwa na majukumu mengi na huenda asiwepo tena jijini Dar es salaam hivyo anaogopa anaweza asiitumikie vizuri klabu yake.
“Sababu kubwa kwasasa nina majukumu mengi ninaweza kuhamia Dodoma kwa hiyo nadhani sitaweza kuitumikia vyema klabu yangu ya Simba lakini pia ningependa kuona klabu ina umoja katika kipindi hiki ambacho tunataraji kutetea ubingwa wetu ambao tuliupata msimu uliopita.” ameeleza.
Mtemi amefafanua kuwa mara nyingi nafasi hizi zimekuwa zikiwagawa wanachama na kupelekea kuleta makundi ambayo yanakuwa hasimu na kuondoa umoja ambao ungepelekea timu kufanikiwa badala inafanya vibaya.
Pamoja na kujitoa lakini Mtemi ametoa rai  kwa wanachama wa klabu hiyo akiwataka wachague viongozi waadilifu na imara ambao watasaidia kuitoa klabu hiyo katika sehemu moja kwenda nyingine hususani kipindi hiki wanachofanya mabadiliko.
Baada ya Mtemi Ramadhani kujiondoa, mchakato huo unabakia na mgombea mmoja pekee katika nafasi ya Uenyekiti ambaye ni Sued Nkwabi.
Wagombea katika nafasi mbalimbali.
UENYEKITI
Sued Mkwabi
WAJUMBE
1) Hussein Kitta Mlinga
2) Iddy Noor Kajuna
3) Zawadi All Kadunda
4) Mohamed Wandi
5) Selemani Harubu Said
6) Abdallah Rashid Mgomba
7) Christopher Kabalika Mwansasu
8) Alfred Matin Elia
9) Ally Suru
10) Mwina Mohamed Kaduguda
11) Said Tully
12) Jasmine Badar Soudy
13) Juma Abbas Pinto
14) Hamis Ramadhani Mkoma
15) Abubakari Zebo
16) Patrick Paul Rweyemamu
17) Asha Ramadhani Baraka.
Walioenguliwa ni:
1) Selemani Omari Selemani
2) Omar Juma Mazola.

Comments are closed.