ONTLAMETSE Phalatse raia wa Afrika Kusini aliyekuwa na ugonjwa wa maumbile, amefariki dunia usiku wa kumkia leo katika hospitali ya Dr, George Mukhari iliyopo nje kidogo ya mji wa Pretoria.
Ontlametse alikuwa ni mmoja kati ya watu wawili waishio Afrika ya kusini waliozaliwa na ugonjwa huo. Kifo hicho kimetokea mwezi mmoja baada ya kukamilisha azma yake ya kukutana na rais Zuma wa nchi hiyo.