The House of Favourite Newspapers

Mgosi ataka kuvunja rekodi ya Kibadeni

0

NAHODHA wa Simba, Mussa Mgosi, leo atacheza dhidi ya Yanga akiwa na mambo mawili kichwani, moja ni kuipatia ushindi timu yake, pili kuvunja rekodi ya Abdallah Kibadeni ya kufunga mabao matatu ‘hat trick’.

Hadi leo, rekodi ya kufunga hat trick katika mechi ya watani wa jadi iliyowekwa na Kibadeni Julai 19, 1977 ambapo Simba iliifunga Yanga mabao 6-0 haijavunjwa.

Kibadeni alifunga mabao hayo katika dakika za 10, 42 na 89. Mabao mengine ya Simba yalifungwa na Jumanne Hassan ‘Masimenti’ dakika za 60 na 73 na lingine lilikuwa la kujifunga la Selewa Sanga wa Yanga dakika ya 20.

Mgosi aliliambia Championi Jumamosi: “Siku niliyoisubiria imefika, nafikiria kuivunja rekodi ya Kibadeni tu katika mchezo wa kesho (leo), maana naona miaka inazidi kwenda tu na hakuna anayejitokeza kuivunja.

“Sisi ndiyo tunatakiwa kuivunja, naamini nitafanya hivyo katika mchezo huu kutokana na kwamba wachezaji wa Yanga nawafahamu vizuri tu na hawanipi shida.”

Hata hivyo, tofauti na Hamis Kiiza anayeongoza kwa ufungaji Simba akiwa na mabao matano na Justice Majabvi mwenye bao moja, Mgosi ambaye ni straika hajafunga hata bao moja katika mechi mbili za ligi alizocheza.

Leave A Reply