The House of Favourite Newspapers

Mgosi haoni beki wa kumzuia Yanga, Kiiza yeye anafunga tu

0

WAKATI Mussa Mgosi wa Simba amesema haoni beki wa Yanga atakayeweza kumzuia katika mchezo wao leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, straika mwenzake Hamis Kiiza yeye anafunga tu.

Mgosi ameliambia Championi Jumamosi kuwa, mabeki wote wa Yanga anawajua uwezo wao na aliwasumbua msimu uliopita akiwa na Mtibwa Sugar, hivyo leo wajiandae kusumbuka tena.

Msimu uliopita akiichezea Mtibwa, Mgosi alifunga bao moja wakati timu yake ilipoifunga Yanga mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro huku bao likifungwa na Ame Ally ambaye sasa yupo Azam FC.

“Mimi nimejiandaa vizuri na mechi hii ya Yanga, beki zao nazijua na nilizisumbua sana nilipokuwa Mtibwa, namjua vizuri Cannavaro (Nadir Haroub) hata Yondani (Kelvin), tena huyo (Yondani) namjua tangu akiwa Simba,” alisema Mgosi.

Wakati huohuo, Kiiza ameonyesha kwamba analijua sana goli kutokana na kuendelea kufunga mabao mazoezini wakati kikosi hicho kilipokuwa kinajiandaa na mchezo wa leo.

Mpaka sasa kwenye ligi, Kiiza amefanikiwa kufunga mabao matano huku akiwa ndiye kinara wa mabao katika ligi hiyo yenye wachezaji zaidi ya 300.

“Kazi yangu ni kufunga na nitaendelea kufunga kila ninapopata nafasi, siwezi kusema mengi zaidi ya hapo, bali tukutane uwanjani,” alisema Kiiza.

Leave A Reply