The House of Favourite Newspapers

Mgosi: Simba Queens itatwaa ubingwa

KOCHA Mkuu wa Timu ya Wanawake ya Simba Queens, Musa Hassan Mgosi amesema licha ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Alliance Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, bado anaamini msimu huu watatwaa ubingwa la ligi hiyo.

Mgosi ambaye ni straika wa zamani wa Simba, amesema: “Malengo yetu tangu kuanza kwa ligi msimu huu ni kuhakikisha tunatwaa ubingwa na kwa jinsi ligi ilivyo kwa sasa tunaamini kwamba tunaweza kufikia malengo hayo.

“Kikubwa ambacho kinaweza kutuzuia labda suala la waamuzi kwa sababu wengi wao hawana ubora unaotakiwa, hivyo tunawaomba TFF wawatumie wale waamuzi wa ligi kuu kuchezesha michezo yetu kwa sababu wale ndiyo wenye uzoefu mkubwa.”

 

Naye Kocha Mkuu wa Alliance Queens, Ezekiel Chobanka amesisitiza kuwa kitendo cha kuifunga Simba Queens kimewapa hamasa ya kufanya vyema kwenye michezo iliyobakia.

Comments are closed.