The House of Favourite Newspapers

Mgunda Ashusha Presha Simba Awataka Mashabiki Kutulia Mechi za Ligi ya Mabingwa

0
Kocha Msaidizi wa Simba, Juma Mgunda akiongea na wachezaji.

KOCHA Msaidizi wa Simba, Juma Mgunda amewataka mashabiki wa timu hiyo kutulia kwa kuwa mikakati yao ya kutaka kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Bara bado haijapoteza mwelekeo kutokana na ushindani mkubwa uliokuwepo.

Mgunda ametoa kauli hiyo wakati Simba ikiwa inakabiliwa na mchezo wa Kombe FA dhidi ya Coastal Union kesho Jumamosi kabla ya kucheza na Singinda Big Stars, Februari 3, mwaka huu kisha kucheza mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Horoya Februari 10, mwaka huu.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mgunda alisema kuwa, wanatambua ugumu wa michuano iliyo mbele yao lakini ni wakati wa mashabiki wa timu hiyo kutulia na kuweza kuwaunga mkono ili waweze kufikia malengo waliojiwekea msimu huu kwenye michuano yote.

“Nadhani ni wakati wa mashabiki kuweza kutupa sapoti kubwa ya kuhakikisha tunaendelea kupambana kulingana na mechi ambazo zipo mbele yetu ili kuweza kufikia malengo ya timu kutokana na kile ambacho tunahitaji kuweza kukipata kutoka katika kila mchezo.

“Ukiangalia ligi bado ngumu na inakuwa na ushindani mkubwa kutokana na wapinzani wetu kujipanga vizuri lakini tumekuwa katika nafasi ya kuanza kampeni ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sababu tunataka kuona kila mchezo tunaweza kushinda kutokana sapoti kubwa ambayo tunaweza kuipata kutoka upande wao,” alisema Mgunda.

Stori na Ibrahim Mussa

BREAKING: MWILI wa MTANZANIA ALIYEFIA VITANI URUSI WAWASILI ‘AIRPORT’ DAR, NDUGU WAANGUA VILIO…

Leave A Reply