The House of Favourite Newspapers

Mhariri wa Magazeti Pendwa ya Global Afanyiwa Surprize – Picha

0
Wafanyakazi wa Global Group wakizungumza jambo na Mhariri wa Magazeti Pendwa, Sifael Paul (kulia) walipomfanyia bonge moja ya surprise, leo ndani ya ofisi ya Global Group, Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

 

SIFAEL Paul, mhariri wa Magazeti Pendwa ya Global Group, leo amefanyiwa bonge moja ya surprise na uongozi wakati akitimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa huku akiwa kwenye nafasi ya uhariri kwa miaka 10.

Mhariri wa Magazeti ya Risasi Mchanganyiko na Risasi Jumamosi, Erick Evarist (kulia) akiongea jambo baada ya kumkabidhi keki, Sifael Paul (kushoto).

Paul kwa sasa anasimamia gazeti la Ijumaa Wikienda ambalo linatinga mtaani kila Jumatatu kwa bei ya shilingi mia nane na Ijumaa ambalo lipo mtaani kila Ijumaa kwa bei ya shilingi 1,000.

….Sifael Paul akisaidiwa kukata keki na Glory Lucas.

Mhariri huyo ambaye amekuwa akifanya kazi kwa weledi akizingatia miiko ya uandishi wa habari alishtushwa na zawadi kibao mezani zilizoletwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group, Eric Shigongo pamoja na keki kubwa ikiwa ni sehemu ya kumpa pongezi ya kumbukizi yake ya kuzaliwa.

Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally akipokea keki kutoka kwa Sifael Paul.

Hafla hiyo ilifanywa makao makuu ya Global Group, Sinza Mori ambapo wafanyakazi walijumuika pamoja kufurahia na kukata keki na kutoa maneno ya kheri kwake.

….Saleh Ally akizungumza jambo.

Saleh Ally ‘Jembe’ amesema kuwa amekuwa akimtazama kwa ukaribu Paul na amegundua kwamba ni mchapakazi muda wote na hagombani na watu bila sababu za msingi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group, Eric Shigongo (katikati) akizungumza jambo kabla ya kuchukua keki kutoka kwa Sifael Paul.

“Mungu akupe hekima na busara uishi maisha mema, nimekuwa nawe kwa muda wa zaidi ya miaka 10 na sijaona ukiwa ni mgomvi zaidi ya kugombana na watu kwenye masuala ya kazi pekee,” amesema.

Paul amesema kuwa hana kitu kikubwa cha kusema zaidi ya asante kwa wote waliomtakia kheri ya kumbukizi ya kuzaliwa.

Mhariri wa Championi Ijumaa, John Joseph Haramba (kulia) akipokea keki.
Mhariri wa Gazeti la Spoti Xtra, Omary Mdose akipokea keki kutoka kwa Sifael Paul.
Leave A Reply