
MAMBO ni moto katika shindano ya Tusua Maisha na Global ambapo droo ya pili imechezeshwa Jumanne ya Julai 2, 2018 ambapo Amiri Bakari, mkazi wa Ubungo National Housing, ameibuka mshindi wa pikipiki.

Amiri ambaye ni mhasibu katika Kampuni ya Maezeki LTD, ametangazwa kuwa mshindi wa pikipiki ya pili, baada ya wiki iliyopita mshindi mwingine, Richard Tanganyika ambaye anafanya biashara ya kuuza genge, naye kujishindia pikipiki.
Akizungumza na Ijumaa mara baada ya kutangazwa mshindi, Amiri amesema amefurahi sana kuibuka mshindi wa pikipiki hiyo na kueleza kwamba anatarajia kuitumia zawadi hiyo, kama mradi wa kumuingizia fedha kupitia mradi wa bodaboda.

“Nimefurahi sana kwa kweli, wala sikutegemea kama nitaibuka mshindi, yaani hapa nimeshapata mradi mwingine, nitaitumia kwa mradi wa bodaboda, nawashauri watu wengine wasome magazeti ya Global kwani ni kweli wanatoa zawadi,” alisema.

Washindi wengine waliong’ara katika shindano hilo, Kenedy Ngubuya mkazi Mombasa, Gongolamboto jijini Dar es Salaam aliyeibuka na zawadi ya dinner set na Daniel Jackson ambaye pia ni mkazi wa Gongolamboto aliyejishindia headphone za kisasa, Beats by Dre.

Mwingine ni Mwita Matogoro mkazi wa Mwenge jijini Dar es Salaam aliyejishindia jezi. Naye meneja wa Kampuni ya Global Publishers, Abdallah Mrisho, amewasisitiza wasomaji kuendelea kushiriki shindano hilo kwani kila mmoja anayo nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali.

“Droo ya kwanza tulishaichezesha wiki iliyopita na Jumatano (Julai 4, 2018) washindi watakabidhiwa zawadi zao na hii ya sasa ni droo ya pili. Kila mmoja anaweza kuwa mshindi, namna ya kushiriki kwenye Shindano la Tusua Maisha na Global, ni rahisi sana.

“Nunua gazeti lolote linalochapishwa na Global Publishers, kati ya Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Spoti Xtra, kisha funua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya namna ya kushiriki.
“Itume namba maalum inayoonekana juu ya kuponi hiyo kwa njia ya meseji mwenda namba 0719386533. Hakikisha unaihifadhi kuponi au gazeti lako kwani litahitajika wakati wa kuchukua zawadi,” alisema Mrisho.
STORI: MWANDISHI WETU, IJUMAA


Comments are closed.