Mhe. Temba Afungukia Kilichompoteza!

Amani Temba ‘Mheshimiwa Temba’

 

Mwana mpotevu kwenye Bongo Fleva, Amani Temba ‘Mheshimiwa Temba’ amefunguka sababu zilizomfanya kupotea kwenye gemu kwa kipindi cha miaka miwili sasa.

 

Akipiga stori na Risasi Mchan-ganyiko, Temba alisema kwa kipindi kirefu alihamishia nguvu katika elimu, familia na biashara huku akiendelea na shughuli zake za kimuziki kimyakimya.

 

“Nilikuwa kimya kwa muda wa miaka miwili kwa sababu mambo yaliingiliana. Nilikuwa ninasoma. Pia ni baba wa familia, mfanyabishara na ninasimamia kundi la vijana. Hayo yote ni majukumu yangu huku nikiangalia maisha yanaendaje,” alisema Mheshimiwa Temba.

Temba alisema kwa sasa amekuja kivingine kwa kuachia ngoma mwisho wa mwaka, ambayo ameifanya nchini Uingereza kulikomsaidia kutoka kisasa na kuongeza ladha kwenye muziki wake.

 

“Bado nipo kwenye game, ngoma yangu mpya itadhihirisha hilo hivyo mashabiki zangu waendelee kunisapoti,” alisema Temba.

Loading...

Toa comment