The House of Favourite Newspapers

Mheshimiwa Beatrice Nyamisango Alivyoshiriki Siku ya Pan African Women Day

0
Mwanzilishi wa Asasi isiyo ya kiserikali ya Human Diginity Foundation (HUDEFO) Sara Pima akizungumza kwenye mkutano huo.

DIWANI wa Viti Maalum jiji la Dar es Salaam, Beatrice Nyamisango jana aliungana na wanawake wanaharakati wenzake walipokuwa wakisherehekea Siku ya Mwanamke wa Afrika ambapo Kauli mbiu yao ilikuwa ni Umuhimu wa Mwanamke katika Sayansi.

Mheshimiwa Beatrice Nyamisago akiwasikiliza kinamama waliokuwa wakitoa hoja mbalimbali kwenye hafla hiyo.

 

 

Hafla hiyo iliyoandaliwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya Human Diginity Foundation (HUDEFO) chini ya Mwanzilishi wake Sara Pima, Shirika la Kimataifa la UNESCO na wadau wengine ilifanyika Jengo la Tanzanite jijini Dar es Salaam.

Mh. Beatrice akizungumza kwenye hafla hiyo.

 

 

Katika hafla hiyo Mheshimiwa Beatrice na wageni wengine walipata nafasi ya kujadiliana mambo mbalimbali yaliyokuwa yakilenga kumkomboa mwanamke na kumuwezesha kwenye somo la sayansi.

Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia Mwanzilishi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation, Wanu Hafidh akisikiliza kiumakini yaliyokuwa yakiendelea kwenye hafla hiyo.

 

Waheshimiwa wengine waliohudhulia hafla hiyo ni pamoja na Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambaye pia Mwanzilishi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation, Wanu Hafidh, Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tanga Mwanaisha Ulenge na wengineo.

Leave A Reply