Mhudumu wa Hoteli Akamatwa na Sare za Polisi Dar – Video

Jeshi la Polisi Kanda Maalum linamshikilia Erick Francis (30) muhudumu wa Hotel ya Sleep Inn na mkazi wa Mwananyamala kwa Kopa kwa tuhuma za kukutwa na sare za Jeshi la Polisi cheo cha koplo, silaha, pingu na nguo nyingine inayofanana na sare ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

 

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa jeshi lilipokea taarifa kutoka kwa msiri kuwa kuna mtu mmoja anatumia sare za jeshi la polisi kuwakamata watu na kuwafunga ping.

 

Aidha mtuhumiwa huyo ameshafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili baada ya kukiri kumiliki sare na vifaa mbalimbali vya jeshi la polisi.

 

VIDEO: MSIKIE KAMANDA MAMBOSASA AKIFUNGUKA

Toa comment