The House of Favourite Newspapers

MIAKA 20 YA CHAKUWAMA, SHEIK MKUU AKABIDHI MISAHAFU 100

 

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akiongea.

KATIKA kusheherekea miaka 20 ya kituo cha watoto yatima kilichopo Sinza-Mori jijini Dar kinachojulikana kwa jina la CHAKUWAMA, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Alhadi Musa,  ametoa pongezi  na usia kwa walezi wa kituo hicho kwa kuwapa malezi bora ya kimwili na kiimani.

Akizungumza katika hafla hiyo, alisema kina mama ni walezi wakuu wa watoto kwa sababu wao ndiyo hukaa na watoto muda mrefu.  Pia alimsifia mwasisi  wa kituo hicho marehemu Khadija na rais mstafum Jakaya Kikwete,  kwa msaada alioutoa kwa kituo hicho.

Sheikh Musa alihitimisha ziara yake hapo kwa kutoa zwadi ya misahafu 100 na maboksi kumi ya tende.

Comments are closed.