MIAKA 20 YA TWANGA PEPETA SHUGHULI YAKE ASIKWAMBIE MTU!

Kosi la Twanga Pepeta likiwa ndani ya Studio za Global TV Online.

WAKATI siku zikiendelea kuhesabika kuelekea maadhimisho ya miaka 20 ya bendi ya African Stars ‘Twanga pepeta’ kiongozi wa bendi hiyo Luiza Mbutu amefunguka kuwa wameendaa shoo babu kubwa itakayowaacha wapenzi wa burudani midomo wazi.

Luiza Mbutu akisaini katika kitabu cha wageni walipowasili kwenye studio za Global Group.

Twanga imepanga kufanya tamasha la kutoa shukrani kwa wapenzi na mashabiki wa muziki wa Twanga Pepeta kwa kuwa pamoja na kuisapoti bendi hiyo kwa takribani miaka 20 toka kuanzishwa kwake, tamasha litakalofanyika Oktober 27 mwaka huu katika ukumbi wa Life Park uliopo Mwenge jijini dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka akisalimiana na Mhariri Mrtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally.

Akiambatana na waimbaji, wanenguaji na wapiga vyombo wa bendi hiyo, wakiwa ndani ya Ofisi za Global Group, Luiza amesema kuwa wameandaa ‘suprise’ kibao zitakazowaacha mashabiki midomo wazi, kwa kuwa wamejichimbia mahali wakijifua kwa nguvu zote kuelekea siku hiyo.

Twanga wakizungumza na waandishi pamoja na wahariri wa Global Publishers.

‘’Tumepanga kufanya maangamizi ya kutisha kuelekea siku hiyo tutakayokuwa tunarudisha shukrani kwa mashabiki na tukiazimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa bendi yetu, licha kupitia changamoto nyingi lakini bado walikuwa nasi katika hizo ‘ups and downs’ ni lazima tuwape shoo bab’ kubwa itakayowafanya wafurahie kuwepo ukumbini hapo,’’ alimaliza Mbutu.

Aidha, meneja wa bendi hiyo Martin Sospeter amewataka wakazi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam na viunga vyake wajitokeze Life Park ili kushuhudia maajabu ya shoo ambayo wameiandaa.

Matukio katika Picha:

Toa comment