Miaka 61 ya Mapinduzi Zanzibar Wanawake Wajasiriamali Pemba Wawezeshwa Kiuchumi
Umoja wa wanawake Tanzania UWT umekabidhi cherehani 10 kwa wanawake wajasiriamali wanaojishighulisha na shughuli za kiuchumi za ushonaji wa nguo katika wilaya ya chakechake kisiwani Pemba ili waweze kujiimarisha kiuchumi
Akikabidhi cherehani hizo Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa mkoa wa kusini Pemba NAadra Ghulam Rashid amesema zoezi hilo ni sehemu ya sherehe za miaka 61 ya mapinduzi Zanzibar akiweka bayana kuwa shabaha ya UWT ni kuhakikisha miaka 61 ya mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yana akisi mapinduzi ya kiuchumi kwa wanawake visiwani humo
Aidha ametoa rai kwa wanawake kuhakikisha wana anzisha miradi ya kijasiriamali ili waweze kujiimarisha kiuchumi
Hata hivyo mjumbe huyo amekabidhi kiasi cha cha shilingi milioni mbili kwa ajili ya kusaidia uwezeshaji wa mitaji kwa wajasiriamali katika wilaya ya chake na mkoani kisiwani Pemba pamoja na shilingi milioni tano ili kusaidia ujenzi wa nyumba za UWT .