The House of Favourite Newspapers

Miaka Miwili ya Rais Samia Yaweka Alama ya Mafanikio Makubwa Katika Sekta ya Masoko ya Mitaji

0

 

Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameweka alama kubwa ya mafanikio katika maendeleo na ustawi wa sekta ya masoko ya mitaji, katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wake.

Akielezea mafanikio makubwa yaliyopatikana, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama amesema, mafanikio hayo yametokana na mazingira wezeshi, shirikishi na endelevu ya kisera, kisheria na kiutendaji ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi madhubuti wa Dk. Samia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkama ameongeza kuwa sera za uchumi wa kidiplomasia na uhusiano wa kimataifa zinazotekelezwa chini ya uongozi wa Rais, zimekuwa chachu yenye matokeo chanya katika kukuza ushiriki wa wawekezaji wa ndani na wakimataifa na hivyo kuleta mafanikio makubwa zaidi katika masoko ya mitaji.

 

Mkama amesema, mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na:

 

  • Thamani ya uwekezaji katika masoko ya mitaji imeongezeka kwa asilimia 18.3 na kufikia shilingi trilioni 35.3 katika kipindi kilichoishia Februari 2023, ikilinganishwa na shilingi trilioni 29.9 katika kipindi kilichoishia Februari 2021;

 

  • Jumla ya mauzo ya hisa na hatifungani yameongezeka kwa asilimia 40.1 na kufikia shilingi trilioni 6.4 katika kipindi kilichoishia Februari 2023, ikilinganishwa na shilingi trilioni 4.6 katika kipindi kilichoishia Februari 2021;

 

  • Mauzo ya hatifungani yameongezeka kwa asilimia 83.2 na kufikia shilingi trilioni 6.1 katika kipindi kilichoishia Februari 2023, ikilinganishwa na shilingi trilioni 3.4 katika kipindi kilichoishia Februari 2021;

 

  • Thamani ya Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja katika kipindi kilichoishia Februari 2023 imeongezeka kwa asilimia 155.28 na kufikia shilingi trilioni 1.42 ikilinganishwa na shilingi bilioni 557.28 katika kipindi kilichoishia Februari 2021.

 

Masoko ya Mitaji Tanzania ni miongoni mwa masoko matano bora yaliyopata mafanikio makubwa kiutendaji barani Afrika, katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Dk. Samia. CMSA, ambayo ni Mamlaka yenye jukumu la kusimamia na kuendeleza masoko ya mitaji hapa nchini imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza mikakati ambayo imeweze- sha kufikia mafanikio hayo.

Mamlaka imetekeleza mikakati ambayo imewezesha kufungua Nyanja na fursa mpya katika masoko ya mitaji. Mikakati hiyo ni pamoja na: kuanzisha bidhaa na huduma mpya, bunifu, zenye mlengo maalum na matokeo chanya kwa jamii; matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika kutoa huduma; kuongeza idadi ya wataalamu wanaokidhi viwango vya kimataifa; na kutoa elemu kwa umma kuhusu fursa zinazopatikana katika masoko ya mitaji.

 

Bw. Mkama pia alisema, kwa mujibu wa taarifa ya Benki ya Dunia kuhusu tathmini ya Utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja katika Jumuiya ya Afrika Mashariki yaani East African Common Market Protocal Scorecard on movement of capital, goods and services, Tanzania imepanda viwango vya alama za tathmini kwa asilimia 157 kutoka alama 7 hadi alama 18 kati ya 20 na kuwa nchi ya pili katika utekelezaji wa itifaki ya soko la pamoja katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa sasa, Tanzania hakuna vikwazo vya ushiriki wa wawekezaji wa kigeni katika soko la hisa, hatifungani za kampuni na mifuko ya uwekezaji wa pamoja.

 

Katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Mhe. Rais Dk. Samia, Mamlaka imetekeleza mikakati ambayo imewezesha kuanzisha bidhaa na huduma mpya bunifu na zenye mlengo maalum wa maadili yaani ethical Sharia Compliant Sukuk bonds na zenye mguso na matokeo chanya kwa jamii yaani social bond. Bidhaa hizo ni pamoja na:

 

  • Hatifungani yenye mguso na matokeo chanya kwa Jamii iliyoitwa NMB Jasiri Bond ambapo kiasi cha shilingi bilioni 74.3 kilipatikana, sawa na mafanikio ya asilimia 297. Hatifungani ya Jasiri imeweka historia ya kuwa hatifungani ya kwanza yenye mguso wa jamii, kutolewa nchini Tanzania na Ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Aidha hatifungani hii imeorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) na Soko la Hisa la Luxemburg (LuxLE). Fedha zilizopatikana zinatumika kutoa mikopo kwa ajili ya kuendeleza biashara ndogo na za kati zinazomilikiwa na kuendeshwa na wanawake, au zile ambazo bidhaa na huduma zake zinamgusa mwanamke.

 

  • Hatifungani inayokidhi misingi ya Sharia inayoitwa KCB Fursa Sukuk, ambapo kiasi cha shilingi bilioni 11 kilipatikana, sawa na mafanikio ya asilimia 110. Hatifungani hii imeweka historia ya kuwa hatifungani ya kwanza inayokidhi misingi ya Shariah kutole- wa kwa umma na kuorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam. Fedha zilizopa- tikana zinatumika kuwekeza katika biashara ndogo na za kati zinazokidhi misingi ya Sharia;

 

  • Hatifungani ya Benki ya NBC yenye thamani ya shilingi bilioni 300 itakayotolewa katika awamu sita. Mauzo ya awamu ya kwanza iliyoitwa NBC Twiga Bond yalifan- yika, ambapo kiasi cha shilingi bilioni 38.9 kilipatikana, sawa na mafanikio ya asilimia
  1. Fedha zilizopatikana zinatumika kutoa mikopo kwa ajili ya kuendeleza kampuni za wajasiriamali wadogo na wa kati katika mnyororo wa thamani wa kilimo biashara;

 

  • Hatifungani aina ya Sukuk iliyotolewa na Taasisi ya Fedha Imaan, ambapo kiasi cha shilingi bilioni 24.03 kilipatikana sawa na mafanikio ya asilimia 146. Fedha zilizopati- kana zinatumika kuwekeza katika biashara ndogo na za kati zinazokidhi misingi ya Sharia;

 

  • Hatifungani aina ya Sukuk iliyotolewa na Benki ya Amana, ambapo kiasi cha shilingi bilioni 6.75 kilipatikana, ikilinganishwa na shilingi bilioni 5 zilizotarajiwa kukusany- wa, sawa na mafanikio ya asilimia 135. Fedha zilizopatikana zinatumika kuwekeza katika biashara ndogo na za kati zinazokidhi misingi ya Sharia.

 

  • Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja unaoitwa Faida Fund, unaoendeshwa na Taasisi ya Watumishi Housing Investments (WHI). Mauzo ya awali ya Mfuko huu yamewezesha kupatikana kiasi cha shilingi bilioni 12.95, ikiwa ni mafanikio ya asilimia 173. Mfuko huu unatoa fursa ya kuwekeza kwa kuanzia shilingi 10,000 hivyo kuwezesha wawekezaji wa kada mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vijana, wanawake, makundi maalum kunufaika na uwekezaji katika masoko ya fedha; kujenga utamaduni wa kuweka akiba; na kuwawezesha wananchi kushiriki katika uchumi.

 

  • Hatifungani kwa ajili ya kuendeleza Sekta ya Nyumba na Makazi iliyotolewa na Kampuni ya Tanzania Mortgage Refinance ambapo kiasi cha shilingi bilioni 8.9 kimepatika- na, sawa na mafanikio ya asilimia 127. Fedha zilizopatikana zimanatumika kwa ajili ya kuendeleza sekta ya nyumba na makazi.

 

Bw. Mkama amesema katika kuboresha na kuimarisha huduma za masoko ya mitaji, Serika- li kupitia CMSA imefanya mapitio ya Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, ambapo kifungu Na. 134A kimeongezwa kwenye Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, Sura 79 ya Sheria za Tanzania.

Maboresho ya Sheria yamepitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muunga- no wa Tanzania, ikiwa ni sehemu ya vifungu vya Sheria vilivyoboreshwa (Miscellaneous Amendments). Maboresho haya yana lengo la kulinda maslahi ya wawekezaji wenye hisa chache katika kampuni za umma na zilizo orodheshwa katika Soko la Hisa, ikiwa ni pamoja na: kuimarisha misingi ya utawala bora kwa kuwa na uwakilishi wa wawekezaji wenye hisa chache kwenye Bodi ya Wakurugenzi na ushiriki wa wawekezaji hao katika kufanya maamuzi kwenye mikutano mikuu ya kampuni.

 

Katika kutumia fursa ya masoko ya fedha ya ndani na ya kimataifa yanayowezesha kupati- kana kwa fedha za kugharamia miradi ya maendeleo inayochangia Utunzaji wa Mazingira, Maendeleo ya jamii na Utawala Bora yaani Environmental, Social and Governance (ESG), CMSA imeidhinisha maboresho ya Kanuni za Soko la Hisa la Dar es Salaam yaani Stock Exchange Rules, ili kuwezesha uorodheshwaji na mauzo ya bidhaa hizo. Maboresho hayo yameongeza mauzo na kuweka mazingira wezesh kwa sekta ya umma na binafsi kupata fedha za kugharamia shughuli za maendeleo.

Aidha maboresho hayo yameongeza matumizi ya bidhaa na huduma, hivyo kuongeza ukwasi kwenye masoko ya mitaji.

Vile vile katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Samia, CMSA imetekeleza mkakati wa kuwezesha utoaji wa Hatifungani za Serikali za Mitaa na Taasisi za Umma yaani Municipal and Subnational Bonds ili kuwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa (Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya) na Taasisi za Umma, ikiwa ni pamoja na Mamlaka za Maji na Mazingira kugharamia miradi ya kimkakati yenye uwezo wa kujiendesha kibiashara.

Jitihada hizi ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Serikali wa njia mbadala za kugharamia miradi ya maendeleo katika sekta ya umma na binafsi yaani Alternative Project Financing Strategy, uliozinduliwa na Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wenye lengo la kuwezesha upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya kujenga uchumi shindani kwa maendeleo ya watu.

Jitihada hizo zimeiwezesha Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Tanga yaani Tanga Urban Water Supply and Sanitation Authority (Tanga-UWASA) kuwa Taasisi ya kwanza nchini kukidhi vigezo vya awali vinavyowezesha kutoa hatifungani kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji na utunzaji wa mazingira yaani the first Sub-National Water Infrastructure Green Revenue Bond.

Katika kuwezesha matumizi ya teknolojia, CMSA ilidhinisha mifumo ya Sim Invest na Hisa Kiganjani ambazo zinawezesha kutoa huduma katika masoko ya mitaji kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano katika kuuza na kununua dhamana. Hatua hii imeweze- sha kuongeza ushiriki wa wananchi mijini na vijijini katika mifuko ya uwekezaji wa pamoja na soko la hisa.

Aidha, CMSA imeshirikiana na wadau kuandaa miongozo ya kuendesha na kusimamia bidhaa za uwekezaji wa makundi yaani crowdfunding. Bidhaa hizi zitawezesha upatikanaji wa fedha kwa kampuni changa, ndogo na za kati yaani startup, micro, small and médium enterprises.

Katika jitihada za kuongeza wataalamu wenye weledi na ujuzi kwa ngazi ya kimataifa kwenye masoko ya mitaji, CMSA kwa kushirikiana na Taasisi ya Uwekezaji na Dhamana ya nchini Uingereza yaani Chartered Institute for Securities and Investment imetoa mafunzo yanayotambulika kimataifa kwa watendaji wa masoko ya mitaji hapa nchini.

Mafunzo haya yamewezesha kujenga uwezo na ufanisi kwa watendaji wa masoko ya mitaji, ambapo idadi ya wataalamu wanaokidhi viwango vya kimataifa imeongezeka kwa asilimia 49.2 na kufikia 737 katika kipindi kilichoishia Februari 2023 kutoka 494 katika kipindi kilichoishia Februari 2021.

Mafunzo haya yamewapatia wataalamu wa masoko ya mitaji fursa ya kupata leseni za kutoa huduma katika masoko ya Kitaifa, Afrika Mashariki na kimataifa. Aidha, mafunzo haya yamewezesha kuongeza idadi ya watendaji wa masoko ya mitaji wenye leseni ya CMSA kutoka 144 na kufikia 166, ikiwa ni ongezeko la asilimia 15.3.

Katika kutoa elimu kwa umma kwa lengo la kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu fursa zinazopatikana katika masoko ya mitaji, CMSA imetoa mada kuhusu fursa zinazopatikana kwenye masoko ya mitaji kwa njia ya machapisho magazetini na mahojiano kwenye vipindi vya redio na runinga; imetengeneza na kusambaza shajara na vipeperushi vyenye elimu ya masoko ya mitaji na dhamana; imechapisha na kusambaza kwa wadau Taarifa ya Mwaka ya Mamlaka ili kutoa elimu na taarifa ya utendaji kazi wa sekta ya masoko ya mitaji; kushiriki katika maonyesho ya kitaifa na kimataifa yenye lengo la kutoa elimu kuhusu fursa na faida

 

za kutumia masoko ya mitaji, ikiwa ni pamoja na Wiki ya Wawekezaji Duniani (world Investor Week); Wiki ya Huduma za Fedha; na maonyesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba); na Kuendesha mashindano kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu kuhusu masoko ya mitaji na uwekezaji. Mashindano hayo yameonyesha mafanikio makubwa kutokana na kuendeshwa kwa kutumia njia ya mitandao ya kielektroniki yaani simu za mikononi na intaneti.

Mashindano haya yamesaidia kuongeza elimu ya masoko ya mitaji kwa vijana wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu, ambapo idadi ya washiriki imeongezeka kutoka wanafunzi 48,662 katika kipindi kilichoishia Februari 2021 na kufikia wanafunzi 70,133 katika kipindi kilichoishia Februari 2023, ikiwa ni ongezeko la asilimia

43.7. Mashindano haya yamekuwa na matokeo chanya kwa kuongeza idadi ya wawekezaji vijana 10,000 katika masoko ya mitaji; kuanzishwa kwa Jukwaa la Wawekezaji Vijana lenye wanachama zaidi ya 6,000 ambalo linawezesha wawekezaji vijana kupata elimu na uzoefu wa uwekezaji katika masoko ya mitaji.

Bw. Mkama alihitimisha kwa kusema kuwa, Sekta ya Masoko ya Mitaji Tanzania ni imara na himilivu na kuwa CMSA itaendelea na jitihada zenye lengo la kuchagiza na kutoa mchango chanya katika kujenga uchumi shindani kwa maendeleo ya watu. Bw. Mkama amemtakia Mheshimiwa Rais Dk. Samia heri katika uongozi wake na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu afya njema, baraka na fanaka katika kutekeleza kazi ya kuleta maendeleo ya jamii na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.

Leave A Reply