The House of Favourite Newspapers

Michelle Obama Kuwania Urais wa Marekani 2020?

 

MICHELLE  ambaye ni mke wa rais wa zamani wa Marekani,Barack Obama, tetesi za yeye kuwania urais mwaka 2020 nchini humo zimeongezeka kutokana na ziara anayoifanya ya kusambaza kitabu chake cha ‘Becoming’ katika miji kumi mikubwa ya kukitangaza kitabu chake hicho.

 

Mbali na ziara yake hiyo ambayo imemkutanisha na watu wengi akiwamo ‘Meghan Markle’ katika kikao cha faragha huko jijini London nchini Uingereza, hatua yake ya wiki chache zilizopita kujitokeza hadharani na kuhamasisha watu wasio na vyama  kupiga kura katika uchaguzi  uliofanyika Novemba 4 mwaka huu wa maseneta na magavana ndiyo unaelezwa kkwaamsha umma na hata baadhi kujenga hisia kuwa Michelle anajiandaa na urais mwaka 2020.

 

 

Inaelezwa kuwa Michelle amekuwa miongoni mwa watu maarufu katika siasa za Marekani, huku kura za maoni zikionyesha ameendelea kuungwa mkono kwa zaidi ya asilimia 60.

 

Uchambuzi wa kura ya maoni ya  Zogby uliotolewa Mei mwaka huu unapendekeza, Michelle pengine angeanza kutumia fursa ya sasa dhidi ya Rais Donald Trump .

 

Kura ya maoni iliyoendeshwa na Zogby inaonyesha Michelle ana asilimia 48 dhidi  ya asilimia 39 za Rais Trump.

Wakati katika kura ya maoni ya yougov.com iliyofanywa mwezi Aprili mwaka huu inaonyesha chama cha Democrat kinapewa asilimia 90 ya kushinda katika uchaguzi ujao.

 

Watu wengi ndani ya chama cha Democrat wanapiga kelele za kutaka Michelle agombee urais 2020.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini humo wamebainisha kuwa Obama anamuongezea nguvu  ya kimaadili Michelle ya kuomba kugombea katika uchaguzi ujao.

 

Kelele hizo za kisiasa zimeongeza kwa kusema wakati nchi ikionekana kuwa vipande-vipande kuliko wakati mwingine, ile sauti ya kuhamasisha ya Michelle nayo inaelezwa kumpa nguvu ndani ya chama cha Democrat na Marekani kwa ujumla kuwania nafasi hiyo ya juu.

 

Wanasema ni sauti ileile ambayo aliitoa wakati akiwa  mke wa rais, na wakati ambao alikuwa akijaribu kuondoka kwenye siasa  akitangaza kujikita kwenye masuala ya afya za watoto na lishe na kusaidia familia za kijeshi.

 

Michael Starr Hopkins, mwanamikakati wa chama cha Democrat na mkongwe  wa kampeni za mwaka 2008 za Rais Obama anasema; “Michelle anapozungumza haonekani kutoka kwenye historia ya siasa lakini anachozungumza  kina ujumbe halisi na watu wanamwamini sana,”

 

Katika uchambuzi wao wa nani anayepaswa kuwa mgombea urais, tovuti hiyo iliyojikita katika chambuzi za maoni ya kisayansi kuhusu siasa, uchumi na michezo ya FiveThirtyEight (538) imechambua kuwa huenda kitabu cha Michelle cha ‘Becoming’  kutoka sasa ni sehemu ya kampeni kuelekea 2020.

 

Zaidi wanasema ni kiashiria kuwa kuna mtu anajipanga kwa ajili ya kuwania urais. Aidha, wapo wanaosema Michelle anajiona hana sifa za kugombea urais.

 

Pamoja na kipaji chake cha uongozi alichonacho, haiba na umahiri wa hotuba zake  za kuhamasisha anasema haguswi na siasa.

 

“Sababu kwa nini sitaki kuwania urais na siwezi kusema kwa Oprah, hisia zangu ni kwamba, kwanza kabisa, unahitaji kazi,” alikaririwa Michelle akisema  katika mkutano wa 39  wa Simmons Leadership.

 

Mamia tayari walijitokeza kwenye mitandao ya kijamii baada ya ushindi wa Trump kumhimiza Michelle awanie urais mwaka 2020.

 

“Mazingira mwafaka sana kwa Michelle Obama kushinda uchaguzi 2020,” mmoja aliandika.

 

Mwingine alisema: “Michelle Obama 2020 tafadhali Michelle Obama 2020 tafadhali Michelle Obama 2020 tafadhali”.

 

Kwa mujibu wa utafiti wa Gallup, Bi Obama anapendwa asilimia 64 na Wamarekani, kiwango kilicho juu ya Donald Trump, Hillary Clinton na hata mumewe.

 

Comments are closed.