The House of Favourite Newspapers

Michirizi Ya Damu – 07

0

“Hujioni? Nenda kachukue kioo halafu jiangalie,” alisema Keith huku akimwangalia Fareed.

“Hapana!”
“Niamini!”

Safari zake za kutafuta wanaume hazikuisha, aliendelea kuizunguka dunia, kila alipoambiwa na wakala wake kwamba kulikuwa na mwanaume aliyekuwa akimtaka, alikwenda huko, alizunguka sehemu mbalimbali na hakutaka kabisa Godfrey ajue kile kilichokuwa kikiendelea katika maisha yake.

“Upo wapi Fareed,” aliuliza Keith kupitia ujumbe mfupi kwenye Mtandao wa WhatsApp.

“Ubelgiji!”
“Nahitaji nikuone.”
“Lini?”

“Hata kesho!”
“Mh! Mbona haraka hivyo?”
“Kwa sbabu nimekumisi.”
“Basi naomba tufanye wiki ijayo. Nitakuja tu rafiki yangu,” alisema Fareed.

“Basi sawa. Nakusubiri kwa hamu!”
“Kuna nini lakini?”
“Hakuna kitu! Nataka nikuone tu.”
“Mmh! Sawa,” alisema Fareed na kukata simu, hakuamini kama kulikuwa na kitu cha kawaida, alijua kabisa kwamba kulikuwa na kitu mwanaume huyo alikuwa akikihitaji kutoka kwake. Hivyo akajiandaa.

****

Bilionea Keith alikuwa nyumbani kwake ametulia, aliyafikiria maisha yake, tangu siku alipopata ufahamu mpaka hapo alipofika. Alipitia mengi, alipata matatizo makubwa lakini yote hayo baadaye yakageuka na kuwa changamoto katika maisha yake.

Alifanya ushenzi wa kila aina kupitia fedha zake. Alitembea na wanawake wa kila aina, alifanya ujinga wote mpaka kuona kwamba hakukuwa na ujinga ambao hakuwahi kuufanya katika maisha yake mpaka sasa.

Aliyatathmini maisha yake na mwisho kugundua kwamba kwenye ushenzi wote aliokuwa ameufanya, kulikuwa na ushenzi mmoja tu ambao hakuwa ameufanya na ndiyo ambao ulimfanya kumpigia simu Fareed na kuomba kuonana naye.

Mwili wake ulimsisimka, hakutaka kuona kitu kingine tena zaidi ya kutembea na Fareed ambaye kwa muonekano wake tu ulimtamanisha kupita kawaida. Siku iliyofuata akampigia simu na kutaka kuonana naye kitu ambacho hakikuwa kigumu kwa Fareed, akamwambia kwamba wiki inayofuata angeonana naye na kutaka kusikia kile alichokuwa amemuitia.

Kuanzia siku hiyo, Keith akawa na mawazo mengi, moyo wake haukutulia, ilikuwa ni kama Fareed alikuwa na majini kwani kipindi cha nyuma alimuona kuwa mtu wa kawaida lakini muda huo alibadilika, alianza kupata nguvu sana moyoni mwake.

Mwanaume tata huyo kila siku akawa akiwasiliana naye na kumuuliza ni kitu gani hicho alitaka kumwambia lakini Keith hakutaka kufumbua mdomo wake na kumwambia zaidi ya kumpa taarifa kwamba angemwambia kama angekwenda nchini Marekani.

“Jamani! Unaniweka kwenye presha mwenzako!” alisema Fareed kwenye simu kwa sauti yake ya kike.

“Usijali! Utakuja na kuona tu,” alisema Keith.

Siku zikakatika na hatimaye siku ya kwenda nchini Marekani ikawadia. Njiani, Fareed alikuwa na mawazo mengi, hakufikiria kitu kuhusiana na mapenzi, alimwamini mwanaume huyo na kwake alikuwa mmoja wa marafiki zake wakubwa.

Ndege hiyo ilichukua saa zaidi ya ishirini ndipo wakafika nchini Marekani, gari la kifahari lilimfuata, likamchukua na kuelekea katika jumba jingine la Keith ambapo huko aliambiwa asubiri na mwanaume huyo angefika siku hiyo.

Lilikuwa jumba kubwa mno, alizunguka katika kila chumba lakini hakuweza kulimaliza, kila chumba alichoingia kilikuwa kikubwa, alitembea mpaka kuchoka hivyo akaamua kwenda kupumzika katika bwawa la kuogelea.

Walinzi waliokuwa humo walikuwa wakimwangalia Fareed. Hawakuelewa kama huyo waliyekuwa wakimwangalia alikuwa mwanaume au mwanamke. Wengi wakahisi kwamba alikuwa mwanamke, kwa jinsi alivyokuwa mzuri na mikogo yake lakini kitu cha ajabu kabisa, kifuani hakukuwa kama mwanamke, kifua chake kilinyooka kama mwanaume.

“Is he a girl?” (ni mwanamke?) aliuliza jamaa mmoja huku akiwa amemtumbulia macho Fareed.

“I don’t know!” (sifahamu) alijibu jamaa mwingine, yeye mwenyewe alivyomwangalia Fareed, hakumuelewa hata kidogo.

Baada ya kukaa kwa saa tatu ndipo Keith akafika nyumbani hapo. Kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kwenda katika chumba alichompangia Fareed na kumkuta huko.

Mapigo yake ya moyo yalikuwa juu, alimwangalia mwanaume huyo, mwili wake ulikuwa ukisisimka kupita kawaida, alijishangaa kwani kipindi cha nyuma hakuwa hivyo, japokuwa alikuwa mwanaume tata lakini kwake bado aliendelea kuwa mwanaume ila kwa siku hiyo alikuwa hoi kabisa.

Akamsogelea na kumkumbatia, mapigo yake ya moyo yalizidi kudunda kwa nguvu kiasi kwamba mpaka Fareed akashtuka kwani haikuwa kawaida kwa mwanaume huyo kuwa katika hali hiyo.

“What the hell wrong with you?” (una nini jamani?) aliuliza Fareed huku akimwangalia Keith.

“I got nothing!” (hakuna chochote)
“No! Tell me the truth!” (Hapana! Niambie kweli)
“That’s the truth! I got nothing. I just missed you,” (huo ndiyo ukweli! Sina kitu, nilikukumbuka tu) alijibu mwanaume huyo huku kwa mbali kijasho chembamba kikianza kumtoka.

Walikaa na kuzungumza mambo mengi, muda mwingi alikuwa akimwangalia Fareed, mapigo yake ya moyo hayakuacha kudunda na kwa jinsi Fareed alivyokuwa na makusudi, akaanza kukaa mikao ya hasarahasara pale kwenye kochi.

Moyo wake ulikuwa kwenye maombi mazito, kila alipomwangalia Fareed jinsi alivyokaa pale kwenye kochi, aliona kabisa shetani alikuwa akimzidi nguvu, tena kwa kasi kubwa.

Alipambana lakini kila alipotaka kujivika ujasiri aliisikia sauti ikimwambia moyoni mwake kwamba kwa nini asimwambie ukweli Fareed na kumpa kile alichokitaka? Lakini wakati akifikiria hivyo, pia upande mwingine, sauti nyingine ikamwambia kwamba hakutakiwa kufanya hicho alichokuwa akikifikiria kwani lilikuwa chukizo mbele za Mungu wa mbinguni.

“Nitaweza kweli kumshinda shetani? Mungu! Sina nguvu zako moyoni mwangu! Kweli nitaweza kumshinda shetani?” aliuliza Keith huku akimwangalia Fareed ambaye hakuuonekana kuwa na wasiwasi pale kwenye kitanda alipokuwa amekaa, ndiyo kwanza akazidi kuvianika vipaja vyake vilivyopakwa losheni na kukolea hasa.

“Haya niambie sasa…” alisema Fareed.

“Umenikumbusha! Kuna kitu nilitaka kukwambia,” alisema Keith huku akimsogelea Fareed kitandani pale.

“Kitu gani?”
“Ninahitaji ukafanyiwe upasuaji!”
“Upasuaji! Wa nini?”
“Uwekewe makalio makubwa na hata kifua chako kitunishwe, kiwe kama cha mwanamke,” alisema Keith huku akimwangalia Fareed.

Hilo ndilo alilokuwa akilitaka, alitamani kuonekana kama mwanamke. Alitamani kubadilisha jinsia yake na kuwa mwanamke lakini alishindwa, aliogopa kwa kuhisi kwamba angeweza kupata matatizo makubwa.

Akakubaliana na Keith kwamba akafanyiwe upasuaji na kuwekewa muonekano wa kike. Fareed akafurahi sana kiasi kwamba akasimama pale alipokuwa na kumfuata Keith kisha kumkumbatia kwa furaha kubwa.

“Kweli?”
“Ndiyo!”

Siku hiyohiyo Keith akawasiliana na Dk. Fabby wa Hospitali ya New Lucas Medical Center ambaye alikuwa mtaalamu wa upasuaji kwa watu waliokuwa wakihitaji kuwekewa muonekano wa jinsi nyingine. Wakakubaliana na hivyo kitu cha kwanza kabisa alichokitaka ni kuonana na huyo mtu.

Fareed akapelekwa hospitalini hapo. Dk. Fabby alipomuona, hakuamini kama mtu huyo alikuwa mwanaume, alimwangalia kwa makini, alionekana kama mwanamke kwa jinsi alivyokuwa akijiweka.

Akamuita ofisini kwake na kukaa kisha kuzungumza naye. Fareed aliulizwa maswali kadhaa ambayo aliyajibu bila kuwa na hofu yoyote ile kitu kilichomfurahisha daktari huyo.

“Na huyu ni bwana wako?” aliuliza Dk. Fabby!

“Hapana! Ni rafiki yangu!”
“Kweli?”
“Ndiyo!”

“Unajua wewe ni mzuri sana!” alisema Dk. Fabby huku akimsogelea Fareed pale alipokaa, akamshika mkono, kijana huyo akashtuka kwani hakutegemea kumuona dakatri huyo akiwa amebadilika ghafla kama alivyokuwa.

“Unataka kufanya nini?” aliuliza Fareed, alijua kile alichokitaka kukifanya daktari huyo ila alimua kumuuliza kama kumtega.

“Dhambi iliyofanya Sodoma na Gomora kuteketezwa kwa moto,” alisema Dk. Fabby huku akimvua shati laini alilolivaa Fareed ambaye naye bila kipingamizi akamsaidia dokta huyo kuliondoa kabisa mwilini mwake.

“Mh! Leo kazi ipo! Kama hii hospitali haitopaa leo kwa ufirauni ninaotaka kuufanya, basi nitakuwa na bahati,” alijisemea daktari huyo huku akimwangalia Fareed, tena wakati mwingine alitoa pumzi nzitonzito.

***

Godfrey alichanganyikiwa, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, moyo wake ulimuuma sana kwani kwa jinsi mambo yalivyokuwa yakiendelea, alihisi kabisa kuna jambo baya nyuma yake.

Alijaribu kumtafuta Fareed kwenye simu, hakuwa akipatikana, alimtumia meseji nyingi sana WhatsApp lakini mwanaume huyo hakujibu, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, akili yake ilimwambia kwamba wakati huo alikuwa na mwanaume mwingine kitandani kitu kilichouchoma moyo wake vilivyo.

Hakutaka kukata tamaa, aliendelea kumtafuta zaidi na zaidi lakini hakufanikiwa hata kumpata. Kwa kuwa aliwafahamu baadhi ya marafiki zake, akaanza kuuliza huko lakini hakupata majibu, kila aliyemuuliza alisema kwamba hakumuona kitu kilichomuuma sana.

Akakosa furaha, hata kula hakuwa akila, mkewe alimshangaa, alihisi kwamba mume wake alikuwa mgonjwa hivyo kumuuliza mara kadhaa juu ya kilichokuwa kikimsumbua lakini hakuwa radhi kukisema.

“Tatizo nini mume wangu?” aliuliza Theresa huku akimwangalia mume wake usoni.

“Moyo unauma sana!” alijibu huku akishika upande wa moyo wake.

“Kwa nini unauma? Umeanza lini kuuma? Twende hospitali,” alisema Theresa huku akimwangalia mume wake ambaye hakuzungumza kitu zaidi ya kukaa kimya tu.

Aliwahi kuumia maishani mwake lakini maumivu aliyoyapata siku hiyo yalikuwa ni zaidi ya maumivu. Hakukuwa na kitu kilichokwenda sawa, muda mwingi alikuwa akihuzunika, alipokuwa akilala, alimuona Fareed akiwa na mwanaume chumbani kitu kilichouchoma moyo wake vilivyo.

“Haiwezekani! Nitamtafuta mpaka nimpate!” alijisemea.

Alichokifanya siku iliyofuata ni kumtafuta kijana mkali wa kompyuta na kuanza kuzungumza naye. Alimwambia dhumuni lake kwamba ni kumtafuta mtu ambaye alikuwa akitumia simu aliyompa namba zake. Mwanaume huyo akachukua na kuziingiza kwenye kompyuta yake.

Ilikuwa kazi kubwa lakini aliona ilikuwa ni lazima kumsaidia mwanaume huyo kwani kwa jinsi alivyoonekana, alihitaji msaada wake kuliko kitu chochote kile.

Alichokifanya jamaa ni kuiweka programu moja iitwayo Hack My Phone kisha kuziweka namba zile. Hilo wala halikuwa tatizo kwani baada ya nusu sana, GPRS ilionyesha mahali alipokuwa Fareed, alikuwa Los Angeles nchini Marekani.

“Nimempata!” alimwambia Godfrey ambaye alimsogelea.

“Yupo wapi?”
“Los Angeles!”
“Sehemu gani?”

Akamwambia sehemu alipokuwa, hilo halikuwa tatizo alichokifanya ni kuchukua maelezo yote na kuiscreen shot eneo alilokuwa Fareed na hivyo kupanga siku ya kwenda Marekani.

“Unakwenda Marekani? Mbona ghafla hivyo?” aliuliza Theresa huku akionekana kuchanganyikiwa.

“Kuna kitu nakwenda kufanya.”
“Kitu gani?”
“Nimesema kuna kitu nakwenda kufanya!” alisema Godfrey kwa sauti kubwa yenye ukali.

Theresa akahisi kwamba kulikuwa na tatizo kubwa hivyo akamuacha mumewe, kitendo cha kumjibu namna ile kilimaanisha kulikuwa na jambo kubwa nyuma yake.

Hakutaka kuzungumza sana, aliogopa kumkorofisha hivyo kumuacha afanye alichotaka kukifanya. Usiku mzima Godfrey hakulala, alichanganyikiwa na kichwa chake alikiona kuwa kizito sana.

Alipokamilisha taratibu zote za safari, hakutaka kuendelea kubaki nyumbani, akaondoka zake kuelekea Marekani. Ndani ya ndege, alikuwa kimya kabisa, alikuwa na mawazo mengi, hata mtu aliyekaa pembeni yake hakutaka kumuongelesha kwani kwa jinsi alivyoonekana, alikuwa mtu wa mawazo tele.

Ndege ilichukua saa ishirini na mbili mpaka kufika nchini Marekani, katika Jiji la New York ambapo akateremka na kuunganisha ndege mpaka jijini Los Angeles katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa LAX na kuteremka.

Akaichukua simu yake, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuiangalia ile picha aliyokuwa ameiscreen shot, picha iliyomuonyesha sehemu ambapo mpenzi wake alipokuwepo. Alipopaangalia vizuri, akaelekea hotelini.

Hakuacha kumtafuta Fareed, aliendelea kumtafuta zaidi lakini hali haikubadilika, ilikuwa vilevile kwamba hakumpata na hata alipomtumia meseji, hazikujibiwa kitu kilichomchanganya zaidi.

“Huyu atakuwa na mwanaume tu! Yaani wewe subiri! Nitaua mtu,” alijisemea. Japokuwa alikuwa amechoka, hata kulala hakuweza kulala, kichwa chake kilivurugwa na ilikuwa ni lazima ajue kitu gani kilikuwa kikiendelea.

****

Baada ya dakika arobaini na tano, kila mmoja alikuwa hoi. Dk. Fabby alimwangalia Fareed, moyo wake ukajisikia hukumu nzito na kulaumiwa kwa kile alichokuwa amekifanya. Hakujua ni shetani gani alimuingia mpaka kumpelekesha namna ile na kuamua kufanya ushenzi mkubwa kama ule.

Alijuta moyoni mwake, alishindwa kumwangalia Fareed, akaelekea choooni. Huko, alibaki akilia kwa maumivu mazito, huzuni kubwa ilimuingia na hakuamini kama ingetokea siku ambayo angefana ushenzi mkubwa kama huo.

Alimlaumu shetani, alimpa tamaa mbaya ambayo ilimfanya kuusaliti moyo wake na Mungu wake. Kule chooni hakutoka haraka, alikuwa akilia kwa majuto makubwa.

Fareed alipoona Dk. Fabby anachelewa kutoka, akausogelea mlango na kuugonga. Daktari huyo alishtuka na kukumbuka kwamba kulikuwa na kazi aliyotakiwa kufaya, hivyo harakaharaka akanawa uso na kutoka nje.

Hakutaka kumchangamkia Fareed, alichokifanya ni kumpeleka kitandani, akamlaza na kisha kumchoma sindano iliyokuwa na dawa ya kuyaongeza makalio yake kidogo na kifua chake, awe na muonekano kama mwanamke mbichi.

“Tayari!” alisema Dk. Fabby huku akimwangalia Fareed.

“Nashukuru mpenzi!” alisema Fareed huku akimshika kidevu Dk. Fabby lakini akajikwepesha.

“Eeh! Jamani una nini?” aliuliza Fareed.

“Nenda nyumbani!”
“Sawa. Lakini usikose kunipigia. Nitakumiss sana,” alisema Fareed, Dk. Fabby hakuzungumza kitu chochote kile, akamuondoa Fareed chumbani humo.

Hilo hakutaka kulijali sana, Fareed ni akaondoka hospitalini hapo. Moyo wake uliridhika kwani hicho ndicho kitu alichokifanya kila siku. Aliuchukia muonekano wake na alipogundua kwamba baada ya siku chache angekuwa na muonekano wa kike, akafurahi zaidi.

Alipofika nyumbani, akaelekea chumbani na kutulia kitandani. Akachukua simu yake na kuanza kumpigia Dk. Fabby lakini mwanaume huyo hakuhitaji mazoea tana.

“Lakini mbona unanikataa?” aliuliza Fareed.

“Naomba uniache!”
“Nikuache upumzike?”
“Yaani uniache moja kwa moja. Usinijuejue,” alisema Dk. Fabby na kukata simu.

Fareed alihuzunika lakini hakuwa na jinsi, hakutaka kuwasiliana na Dk. Fabby kwani hakumpenda kama alivyompenda Keith ambaye alikuwa tayari kumpa kiasi chochote cha fedha japokuwa hakutaka kumwambia ukweli.

“Haina shida.”
ITAENDELEA SIKU YA KESHO

Leave A Reply