The House of Favourite Newspapers

Michirizi Ya Damu – 09

0

Ndani ya dakika kumi, simu ya Fareed ikalia kuonyesha kwamba kulikuwa na ujumbe, haraka sana akaichukua na kuangalia, ilikuwa ni meseji kutoka katika huduma ya kibenki ambayo ilimwambia kwamba alikuwa amepokea kiasi cha dola elfu hamsini, zaidi ya milioni mia moja na nusu kwa fedha za Kitanzania.

Akakaa chini, hakuamini kile alichokuwa amekiona, hakujua kama alitumiwa na mwanaume ambaye alimpuuzia kila alipomwambia kwamba walitakiwa kuonana. Kiasi hicho kilikuwa kikubwa sana kwake, kwa kawaida aliwatoza wanaume kiasi cha dola elfu moja mpaka elfu mbili, kitendo cha kupewa kiasi kikubwa cha fedha kilimchanganya. Wakati akiwa kwenye hali ya furaha, Mickey akampigia simu.

“Nadhani umeona mabadiliko kwenye akaunti yako!” alisema Mickey.

“Nimeona mpenzi!”
“Huo ni mwanzo. Na nimekupa kiasi kidogo kwa sababu tu huniamini!” alisema Mickey.

Kichwa cha Fareed kilichanganyikiwa, hakuamini kama kweli mwanaume huyo alikuwa amemtumia kiasi kikubwa cha fedha. Hapo ni kwamba hawakuwa wamekutana na kuzungumza, hawakulala kitandani alimgawia kiasi hicho cha fedha, kama angemfanyia kama wengine angepata kiasi gani?

Alipojiuliza, akajikuta akianza kuvutiwa na Mickey. Hakutaka kubaki hotelini, haraka sana anawasiliana na mwanaume huyo kwa miadi ya kuonana na kumwambia kwamba walitakiwa kuonana sehemu tulivu, katika ufukwe wa Kite uliokuwa Magharibi mwa mji huo.

Ndani ya saa moja, tayari Fareed alifika mahali hapo. Alikuwa akiangalia huku na kule akimtafuta mwanaume aliyekuwa amepanga naye miadi ya kuonana.

Baada ya dakika kadhaa, akaliona gari la kifahari, Bugatti la watu wawili likifika mahali hapo. Alilikodolea macho, lilikuwa gari la gharama kubwa na ilionyesha kwamba mtu aliyekuwa humo ndani hakuwa wa mchezomchezo kuhusu masuala ya pesa.

Mlango ukafunguliwa, ukafunguka kwa kwenda juu na mwanaume mmoja aliyevalia suti kuteremka. Watu wote waliokuwa katika ufukwe huo walikuwa wakimwangalia, hawakuamini kama kijana mdogo aliyeteremka ndiye aliyekuwa akiendesha gari hilo la kifahari.

“Mmh! Kuna watu wana hela bwana!” alijisemea Fareed, hakuwa amejua kwamba mwanaume huyo ndiye alikuwa Mickey aliyekuwa akimsubiri.

Moja kwa moja Mickey akaifuata meza ya chakula iliyokuwa katika eneo la kulia chakula, akachukua simu yake na kumpigia Fareed kwa ajili ya kumpa taarifa kwamba alikuwa amefika.

“Mbona sikuoni?” aliuliza Fareed.

“Unaliona hilo gari lililosimama hapo ufukweni?”

“Ndiyo! Hili la kifahari?”
“Yaap!”
“Sasa wewe upo wapi?”
“Umemuona dereva aliyeteremka?”
“Ndiyo!”
“Huyo ndiye mimi!”
“Ndiye wewe? Unaendesha Bugatti?”
“Yeah! Naomba unifuate! Bila shaka unajua hapa nilipokuja kukaa,” alisema Mickey na kisha kukata simu.

Fareed hakuamini, alimdharau mwanaume huyo lakini kumbe alikuwa bilionea mkubwa tu. Wakati anapiga hatua kuelekea kule kulipokuwa na meza ile, macho yake hayakuacha kuliangalia gari lile, lilimpagawisha na kujiona kama yeye ndiye mmiliki halali.

Alipofika katika meza hiyo, kitu cha kwanza Mickey akasimama na kumkumbatia. Ilikuwa vigumu kuamini kama mtu huyo alikuwa mwanaume kwani alivalia gauni refu, kilemba na nyuma alijazia kwani zile sindano alizokuwa amechomwa zilifanya kazi vizuri na hata kifua chake kilijaa.

“U mzuri sana,” alisema Mickey huku akimkumbatia Fareed.

“Nashukuru sana mpenzi!” alisema Fareed, akatoa tabasamu la kike na kutulia kwenye kiti.

Walizungumza mambo mengi huku Mickey akimwambia kwamba alikuwa bilionea kutoka nchini Australia na alifika hapo kwa ajili ya mambo yake ya biashara ila alipomuona klabu siku za nyuma ndizo zilimpagawisha na kuitafuta namba yake ambayo kwa maelezo yake alimwambia kwamba aliinunua kutoka kwa mtu kwa dola elfu mbili.

“Jamaniiiii!”
“Ndiyo ukweli!”

Walizungumza mambo mengi mno huku muda wote Mickey akizungumza kama bilionea mkubwa. Walichukua saa moja, walipomaliza, wakaelekea katika Bugatti ile, wakaingia na kuondoka mahali hapo.

Njiani, Fareed alipagawa mno, moyo wake ulijuta kutofahamiana na mwanaume huyo tangu kitambo kwani alikuwa mzuri wa sura na kubwa zaidi ni kwamba alikuwa na pesa kitu kilichokuwa ugonjwa wake mkubwa kama mtu aliyezaliwa benki.

Wakafika hotelini, Mickey hakutaka kuwa na haraka, aliamini kwamba huyo alikuwa wake hivyo alichokiifanya ni kumuacha huku akimpa dola elfu mbili na kuondoka zake pasipo kufanya kitu chochote kile.

Fareed alichanganyikiwa, alipoingia hotelini, kichwa chake kilikuwa kikimfikiria mwanaume huyo tu. Hakuamini kama kweli alikuwa amefanikiwa kuwa na mtu aliyekuwa na pesa, ambaye hakuwa mchoyo kama alivyokuwa Mickey.

Akaanza kuwa msumbufu, kila wakati alikuwa akimpigia simu mwanaume huyo na kumuuliza alikuwa akiendeleaje, alitaka kuonana naye na kumpa haki yake na si kutumia pesa zake tu.

“Tutaonana tu mpenzi kabla sijarudi Australia! Utakuwa na nafasi usiku wa leo nikufuate twende klabu?” aliuliza Mickey.

“Yeah! Tena nitakuwa mpweke sana. Naomba uje kunichukua mpenzi!” alisema Fareed.

“Sawa. Nitakuja!” alisema Mickey na kukata simu.

Usiku huohuo Mickey akafika hotelini hapo, hakutaka kuchelewa, akamchukua Fareed na kuondoka naye. Walizungumza kama wapenzi, aliongea kama mwanamke na hata mapozi aliyokuwa akiyafanya pale kitini alipokaa alikuwa kama mwanamke.

Saa 8:12 usiku Mickey akamrudisha Fareed hotelini na kisha kuondoka zake. Njiani, hata kabla hajafika katika hoteli aliyochukua chumba, akachukua simu yake na kupiga upande wa pili ambapo baada ya sekunde kadhaa, ikapokelewa.

“Umefikia wapi?” iliuliza sauti ya upande wa pili.

“Kila kitu kipo poa. Kama itawezekana basi kesho tumuue,” alisema Mickey.

“Haina shida. Waambie wenzako kesho mfanye hayo mauaji! Au subiri mpaka nije. Kesho jioni nitaingia, nitahakikisha namuua kwa mkono wangu,” alisema mwanaume upande wa pili na kisha kukata simu.

***

Keith hakutaka kubaki nchini Marekani, aliamini kwamba kwa namna moja au nyingine ilikuwa ni lazima Fareed afe kama alivyokuwa amepanga hivyo ilikuwa ni lazima aondoke na kuelekea Dubai.

Njiani, kichwa chake kilikuwa kikimfikiria mwanaume huyo, aliuumiza moyo wake vilivyo, alitumia kiasi kikubwa cha fedha kumlea lakini kama kunguru vile alishindwa kufugika kabisa.

Aliamua kwamba iwe isiwe ilikuwa ni lazima kumuua ili kuupa furaha moyo wake. Wakati mwingine aliiona ndege ikienda taratibu sana, alitamani hata kuiongezea kasi kwani ilikuwa ni lazima afike mapema, amuue Fareed na kurudi zake nchini MArekani.

Baada ya saa zaidi ya ishirini, ndege ikatua uwanja wa ndege ambapo moja kwa moja akaondoka na kuelekea hotelini. Akawasiliana na Mickey, kijana wake aliyempa kazi ya kufanya mauaji na kumwambia kwamba ilikuwa ni lazima waonane hotelini na vijana wenzake kwa ajili ya kupanga ni kwa namba gani wangeweza kufanya mauaji hayo.

Ndani ya dakika ishirini, vijana wote walikuwa hotelini humo. Akazungumza nao na kuwaambia mipango iliyokuwepo, wakajadili ni kifo cha namna gani mwanaume tata huyo alitakiwa kufa, wakakubaliana kwamba ilikuwa ni lazima abakwe, aingizwe kwenye boti, iende katikati ya bahari huku akiwa amefungwa miguu kwa jiwe kubwa kisha kufa hukohuko.

“Sawa. Wewe endelea kuwasiliana naye,” alisema Keith.

Hapo akawa na amani moyoni mwake, Mickey hakuwa na hofu alijua kwamba Fareed hawezi kutoka mikononi mwake hivyo ilikuwa ni lazima kufanya kama alichoambiwa.

Ili kumtia mshawasha Fareed, siku hiyo alizima simu siku nzima kitu kilichomnyima raha Fareed na kumpigia kila wakati lakini simu haikuweza kupatikana.

Ilipofika saa moja usiku na Fareed kupiga simu, ikawa inaita, mapigo yake ya moyo yakawa juu, hakuamini kama kweli simu hiyo ilikuwa hewani. Alikumbuka Mickey, hakujua kama mwanaume huyo alikuwa mtu mbaya aliyetaka kumuua baada ya kumbaka yeye na wenzake.

Kitendo cha Mickey kupokea simu, Fareed akaanza kuongea kwa sauti ya kulialia kwani alitaka abembelezwe sana, apozwe kama mwanamke aliyekuwa akihitaji faraja kutoka kwa mwanaume aliyekuwa akimpenda kwa dhati.

“Nisamehe mpenzi! Nilikuwa sehemu fulani hivi,” alisikika Mickey kwenye simu.

“Nimekukumbuka jamani! Mpaka nikataka nijiue kwa ajili yako,” alisema Fareed kwa sauti yake ya kuwapagawisha wanaume.

Wakazungumza mengi na mwisho wa siku wakakubaliana kwamba lingekuwa jambo jema kama wangekutaka katika Klabu ya Dubai Night kwa ajili ya kuburudika na kuzungumza mengi. Hiyo ilikuwa furaha kwa Fareed kwani kitu pekee alichokuwa akikitaka kwa kipindi hicho ni kuonana na mwanaume huyo tu.

“Nakuja bebi!”

“Sawa.”

Leave A Reply