Michuano ya Kimataifa ya Kricket Kuanza Kutimua Vumbi Hapa Nchini Kesho

Dar es Salaam, 1 Agosti 2024: Michuano ya Kimataifa ya Kricket ya Wavulana wa chini ya umri wa miaka 19 itaanza kutimua vumbi kesho katika Viwanja vya Gymkhana hapa jijini.
Akizungumza na wanahabari jiji leo Mratibu wa michuano hiyo Atif Salim amesema michuano hiyo itashirikisha timu kutoka mataifa manane ambayo ni Tanzania ambao ndiyo wenyeji, Malawi, Mozambique, Nigeria, Ghana, Botswana, Sierra Leon na Rwanda.

Atif amesema katika timu mbili kwenye makundi mawili yaliyogawanywa kwenye timu hizi yataingia nusu fainali na washindi kati ya hapo wanaingia fainali.
Amesema timu itakayoingia fainali itakuwa imesonga mbele na kufuzu kwenda Divisheni One kabla ya fainali ya michuano hiyo kutakuwa na mechi ya kumtafuta mshindi wa tatu ambapo mshindi huyo atakuwa ni mshindi wa mwisho wa kupata divisheni one.

Mratibu huyo alimalizia kwa kusema fainali hiyo inatarajiwa kupigwa tarehe Agosti 11 mwaka huu ambapo pamoja na Uwanja wa Gymkhana uwanja mwingine utakaotumika ni wa Chuo Kikuu cha Mlimani (UDSM).

Kwa upande wake kocha Msaidizi wa timu ya Tanzania, Salum Jumbe amesema wao kama wenyeji watatumia uzoefu wa kuyazoea mazingira ikiwemo ikiwemo viwanja kuwaweza kuibuka washindi kwenye michuano hiyo.