The House of Favourite Newspapers

Michuano ya Kombe la Dunia Kuaanza leo Jumapili nchini Qatar, Thamani ya Vikosi

0

MICHUANO ya Kombe la Dunia inaanza leo Jumapili nchini Qatar ikishirikisha mataifa 32, huku Afrika ikiwakilishwa na nchi tano; Tunisia, Morocco, Ghana, Senegal na Cameroon.

 

Lakini wakati michuano hii ikianza, kikosi gani ni ghali zaidi? Pia kipi ni kikosi bora ndani ya michuano hiyo?

 

Timu kama Costa Rica, Saudi Arabia, Tunisia, Iran na Australia, katika michuano hii thamani zao zinaonekana kuwa ndogo na hata kuzidiwa thamani na Kylian Mbappe.

 

Wachezaji kama Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, Gareth Bale na Luka Modric, thamani zao zimeshuka hasa kutokana na umri.

 

Kuna mataifa ambayo wana wachezaji wadogo zaidi na thamani zao zipo juu. Mfano kama Phil Foden (England) na Jamal Muisala (Ujerumani).

Kikosi cha timu ya Taifa ya Ufaransa.

 

Safari hii timu za Ulaya na Amerika Kusini zinaonekana kuwa juu katika michuano hii.

Katika makala haya tunaangalia kila kikosi ambacho kinashiriki michuano hii na thamani zao na mchezaji gani ni ghali kwa kila kikosi.

 

32. Qatar – Euro 14.9m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 575,000

Mchezaji mwenye thamani: Akram Afif (Euro 4m)

 

31. Costa Rica – Euro 18.75m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 721,000

Mchezaji mwenye thamani: Keylor Navas (Euro 5m)

 

30. Saudi Arabia – Euro 25.2m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 969,000

Mchezaji mwenye thamani: Sultan Al-Ghannam (Euro 2.5m)

Kikosi cha timu ya Taifa ya England.

 

29. Australia – Euro 38.4m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 1.48m

Mchezaji mwenye thamani: Matthew Ryan (Euro 5m)

 

28. Iran – Euro 59.53m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 2.38m

Mchezaji mwenye thamani: Mehdi Taremi (Euro 20m)

 

27. Tunisia – Euro 62.4m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 2.4m

Mchezaji mwenye thamani: Ellyes Skhiri (Euro 13m)

 

26. Ecuador – Euro 146.5m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 5.63m

Mchezaji mwenye thamani: Moises Caicedo (Euro 38m)

 

25. Japan – Euro 154m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 5.92m

Mchezaji mwenye thamani: Daichi Kamada (Euro 30m)

 

24. Cameroon – Euro 155m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 5.96m

Mchezaji mwenye thamani: Frank Anguissa (Euro 38m)

 

23. Wales – Euro 160.15m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 6.16m

Mchezaji mwenye thamani: Ben Davies & Brennan Johnson (Euro 20m)

 

22.  Korea Kusini – Euro 164.48m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 6.33m

Mchezaji mwenye thamani: Son Heung-min (Euro 70m)

 

21. Mexico – Euro 176.1m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 6.77m

Mchezaji mwenye thamani: Edson Alvarez (Euro 35m)

 

20. Canada – Euro 187.3m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 7.2m

Mchezaji mwenye thamani: Alphonso Davies (Euro 70m)

 

19. Ghana – Euro 216.9m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 8.34m

Mchezaji mwenye thamani: Thomas Partey (Euro 38m)

 

18. Morocco – Euro 251.1m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 9.66m

Mchezaji mwenye thamani: Achraf Hakimi (Euro 65m)

 

17. Poland – Euro 255.6m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 9.83m

Mchezaji mwenye thamani: Robert Lewandowski (Euro 45m)

 

16. Marekani – Euro 277.4m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 10.67m

Mchezaji mwenye thamani: Christian Pulisic (Euro 38m)

 

15. Uswisi – Euro 281m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 10.81m

Mchezaji mwenye thamani: Manuel Akanji (Euro 30m)

 

14. Senegal – Euro 288m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 11.08m

Mchezaji mwenye thamani: Sadio Mane (Euro 60m)

 

13. Denmark – Euro 353m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 13.58m

Mchezaji mwenye thamani: Pierre-Emile Hojbjerg (Euro 45m)

 

12. Serbia – Euro 359.5m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 13.83m

Mchezaji mwenye thamani: Dusan Vlahovic (Euro 80m)

 

11. Croatia – Euro 377m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 14.5m

Mchezaji mwenye thamani: Josko Gvardiol (Euro 60m)

 

10. Uruguay – Euro 449.7m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 17.3m

Mchezaji mwenye thamani: Federico Valverde (Euro 100m)

 

9. Ubelgiji – Euro 563.2m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 21.66m

Mchezaji mwenye thamani: Kevin De Bruyne (Euro 80m)

 

8. Uholanzi – Euro 587.25m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 22.59m

Mchezaji mwenye thamani: Matthijs de Ligt (Euro 70m)

 

7. Argentina – Euro 633.2m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 24.35m

Mchezaji mwenye thamani: Lautaro Martinez (Euro 75m)

 

6. Ujerumani – Euro 855.5m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 34.06m

Mchezaji mwenye thamani: Jamal Muisala (Euro 100m)

 

5. Hispania – Euro 902m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 34.69m

Mchezaji mwenye thamani: Pedri (Euro 100m)

 

4. Ureno – Euro 937m

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 36.04m

Mchezaji mwenye thamani: Rafael Leao (Euro 85m)

 

3. Ufaransa – Euro 1.06b

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 41.63m

Mchezaji mwenye thamani: Kylian Mbappe (Euro 160m)

 

2. Brazil – Euro 1.14b

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 43.92m

Mchezaji mwenye thamani: Vinicius Junior (Euro 120m)

 

1. England – Euro 1.26b

Wastani wa thamani ya mchezaji: Euro 48.46m

Mchezaji mwenye thamani: Phil Foden (Euro 110m)

EXCLUSIVE: ALIKIBA AFUNGUKA KUHUSU DIAMOND KUTOA WIMBO BAADA YAKE – “MI SIKEREKI HATA KIDOGO”

Leave A Reply