SIMANZI, vivlio na majozni imetawala wakati wa kuaga miili ya Watanzania 13 ambao ni ndugu wa familia moja waliofariki kwenye ajali mbaya ya gari iliyotokea nchini Uganda hivi karibuni.
Miili ya wanafamilia hao imeagwa leo Septemba 20, 2017 katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi ya Lugalo jijini Dar es Salaam na baadaye kusafirishwa kuelekea Arusha, Kilimanjaro na Mpwapwa kwa ajili ya mazishi.
Katika ibada hiyo ya kuwaaga marehemu, viongozi mbalimbali wa serikali walikuwepo wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala), Angela Kairuki, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles John Mwijage, Waziri Maalum wa Kusimamia Jiji la Kampala, Betty Kamya kutoka Uganda aliyemwakilisha Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni kukabidhi miili ya marehemu kwa ndugu zao.
Aidha Majeruhi wa ajali hiyo walipelekwa katika Hospitali ya Nkozi na Double Cure Clinic zilizopo nchini Uganda.
Tukio hilo lilimgusa pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyetumia salamu za rambirambi aliyewahi kuwa Naibu Waziri na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Mpwapwa Mkoani Dodoma Bw. Gregory Teu kufuatia vifo vya watu hao ambao ni ndugu wa familia yake.