Miito ya Bamba Tanzania Ndiyo Mchongo wa Mjini

RAHA ya soka lolote duniani ni makelele, iwe nje au ndani ya uwanja, watu wengi sana upenda na usikia raha pale timu asiyoipenda inapofanya vibaya.

Hilo lipo sana hapa kwetu Bongo, hususan kwenye timu za Simba na Yanga ambazo ndiyo nguzo ya soka la nchi hii. Mtu wa Simba usikia raha isiyo na kipimo pale Yanga inapopitia magumu.

Vivo hivyo kwa mtu wa Yanga, siku yake uisha vizuri mno Simba anapochapika. Matambo yanakuwa mengi sana, tambo hizo uwa ni kero kwa shabiki ambaye timu yake itakuwa imefungwa.

Huku kero hiyo uwa furaha na starehe kubwa kwa shabiki ambaye timu yake imetakata kwa wakati huo. Ushahidi wa hayo mambo yapo mitandaoni hasa Global Tv Online.

Huko kuna mashabiki wanajua kuwakera wenzao. Sasa basi kutokana na sababu hiyo Kampuni ya Bamba Tanzania wakaamua kurahisisha mchongo kwa mashabiki wote ambao wanapenda kuwakera wenzao.

Kwa kuwaletea huduma ya miito ya simu ‘Caller tunes’ ambayo itakuwa inampa urahisi shabiki wa Simba kumpa kero shabiki wa Yanga ambaye yupo mbali. Au shabiki wa Yanga kumuhudhi kwa makusudi shabiki wa Simba.

Wakatengeneza kitu kinaitwa Bamba Miito Bomba, ambacho kinapatikana kwa huduma ya mtandao wa simu. Yaani mtu anaweza akampelekea kero ya kishabiki mtu ambaye atakuwa anampigia simu.

Yaani shabiki atasikia timu yake ikitambiwa kwa njia miuito wa simu, kama vile ambavyo baadhi ya watu walivyoweka nyimbo za Bongo Fleva kwenye simu zao.

Huduma hii kwa sasa watumiaji wa Tigo Pesa ndiyo ambao wananufaika. Kwani wakipiga *148*53*2# wataingia kwenye Menu moja kwa moja ambayo itawapa maelekezo ya jinsi ya kujiunga.

Kisha mteja atachagua muito anaoutaka na atalipia shilingi 1,000, pesa ambayo itadumu kwa mwezi mmoja. Lakini itamchukua muda wa masaa 24 hadi kuunganishwa na huduma hiyo.

Hiki ni kitu cha kipekee ambacho kinaonyesha uzalendo na ushabiki wa dhati wa timu yako. Jaribu sasa kujiunga na huduma hii ili uweze kufurahia maisha ya kero kwa shabiki wa timu ambayo wewe hauishabikii.

Tembelea instagram, Facebook na twitter ya Bamba_Tanzania ili uweze kujua mengi mazuri kuhusu huduma hii. Cha kuzingatia ni kwamba mchongo huu ni kwa watumiaji wa Tigo Pesa pekee.

Issa Liponda2181
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment