The House of Favourite Newspapers

Miji 5 Iliyopotea Zama za Kale Yaonekana

1. Helike
Huu ni mji unaokisiwa kuwa ndiyo Atlantis ambao uliteketezwa kwa hasira ya Poseidon — mungu wa baharini kwa Wagiriki.  Uliharibiwa  mwaka 373 Kabla ya Kristo na kuja kugunduliwa mnamo miaka ya 1980 nchini Ugiriki.

2. Xanadu
Xanadu (au Shangdu) ulikuwa makazi ya mfalme wa China, Kubla Khan na mabaki yake yaliyotokana na kuangamizwa kwake mwaka  1369 yamegunduliwa.

3. Sigiriya
Huu ulikuwa makazi ya Mfalme Kassapa wa Sri Lanka ya leo mnamo karne ya tano. Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamadun (UNESCO) liliutangaza Sigiriya kuwa Maajabu ya Nane ya Dunia.

4. Vinland
Haya yalikuwa makazi ya wapiganaji wa Vikings ambapo mabaki yake yaligunduliwa huko Newfoundland, Canada.  Makazi hayo yalijengwa mnamo karne ya 11.

5. La Ciudad Blanca
Huu ni mji uliojulikana kama “Mji Mweupe” wa “Mji wa Mungu Tumbili”.  Mabaki yake yako Honduras, kusini mwa Bara la Amerika.

Comments are closed.