VIDEO: Mikanda ya Ubingwa wa Ndondi wa Global TV Afrika Mashariki na Kati Hadharani
BAADA ya miaka sita kupita bila ya Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem, Dar kutumika katika mchezo wa Msamsumbwi, bondia Nasibu Ramadhan ‘Pacman’ atakuwa ni miongoni wa mwa mabondia watatu wa Tanzania watakaouwasha moto katika mapambano ya Kimataifa la kugombania ubingwa wa Global TV, Afrika Mashariki na Kati kwenye ukumbi huo.
Katika mapambano hayo yatayopigwa Julai 22, mwaka huu kwenye ukumbi huo wa Dar Live na kurushwa mubashara na kituo cha Global TV Online kupitia tovuti ya www.globaltvtz.com, Pacman atacheza na Mzimbabwe, Tinashe Mwadziwana ‘The Chairman’ wakati Francis Miyeyusho ataonyeshana umwamba na Israel Kamwambwa raia wa Malawi huku Idd Pialali akitarajia kumalizana na Regin Champion kutoka DR Congo.
Mtayarishaji wa mapambano ya ndondi hapa nchini, Yassin Abdallah ‘Ustaadh’ amebainisha kuwa, mikanda watakayopewa washindi wa mtanganange huo tayari ipo na kuwaasa wapenzi wa boxing wajitokeze kuutazama mchezo huo bure.
“Mchezo huu utakuwa bure, zitatolewa kadi maalum kwa watu 200 pekee ambao wataingia kutazama, wengine wote watautazama mchezo huo bure kabisa kupitia YouTube Channel ya Global TV Online,” alisema Ustaadh.
Ili kulishuhudia pambano hilo kwa njia ya simu tena bure, hakikisha unajiunga (subscribe) na YouTube Chanel ya Global TV Online sasa hivi ili usipitwe. Ingia You Tube, tafuta GLOBAL TV ONLINE, kisha bonyeza neno subscribe pia bonyeza kikengele kidogo kilichopo pembeni yake ambacho kitakukumbusha kuangalia pambano hilo mara tu litakapoanza.
Kama wewe umeshajiunga, basi hakikisha pia umebonyeza kikengele ili usipitwe na kila kinachoendelea Global TV. Pia unaweza kutupata kupitia mtandao wetu wa www. globaltvtz.com. Usisubiri, jiunge sasa na Global TV ili uwe wa kwanza kuona ndondi za kimataifa.
JIUNGE SASA kwa kubonyeza HAPA: www.youtube.com/ user/uwazi.