The House of Favourite Newspapers

Mikasa na Thamani ya Kombe la Dunia Kutoka Kutengenezwa Hadi Kuibiwa

0
Kombe la Dunia

MNAMO tarehe 20 mwezi Machi 1966 ulikuwa ni mwaka ambao michuano ya kombe la dunia ilifanyika huko nchini Uingereza, lakini kabla ya michuano hiyo kufanyika kulitokea tukio ambalo liliwaacha wengi midomo wazi baada ya kombe la dunia kuibiwa.

 

Mara baada ya kombe hilo kuibiwa lilikuja kugunguliwa na mbwa aliyekuwa akitumika katika upelelezi aitwaye Pickles siku 7 baada ya kuibiwa likiwa limefungwa kwenye gazeti moja hivi huko jijini London, Uingereza.

 

Mikasa ya kuibiwa kwa kombe la dunia haikuishia hapo kwani, mnamo mwezi Desemba 19, 1983 kombe hilo liliibiwa tena ambapo baadaye wanaume wanne walihukumiwa baada kushukiwa kuliiba kombe hilo, lakini licha ya hukumu hiyo kutolewa kombe hilo halikupatikana na baadaye ilisemekana kwamba kombe hilo liliyeyushwa na kuuzwa kutokana na kuwa na ujazo mwingi wa dhahabu.

 

Kutokana na tukio hilo la kuibiwa kwa kombe hilo, Shirikisho la Mpira dunianii FIFA, waliamua kuagiza nakala au ‘copy’ ya Kombe la dunia ili liweze kukabidhiwa kwa mshindi wa michuano hiyo kwa mwaka huo, Kombe hilo lilitengenezwa na Eastman Kodak kwa kutumia Kilo 1.8 za Dhahabu na ndipo lilipobadilishwa jina na kuitwa FIFA World Cup kutoka World Cup au Coupe du Monde na ndilo kombe ambalo linaendela kutumika hadi hii leo kwa mshindi wa michuano hiyo ya kombe la dunia.

Leave A Reply