The House of Favourite Newspapers

Mikate Waliyooka Binadamu wa Kale Yagundulika Jordan

0

KIKUNDI cha wanaakiolojia kimesema wamegundua kwamba binadamu walianza kuoka mikate ya nafaka pori mapema zaidi kabla ya kuanza shughuli za kilimo.

 

Utafiti uliotolewa kwenye Jarida la PNAS la Marekani unaonesha kuwa wanaakiolojia wamegundua mabaki ya mikate ya kuokwa yenye historia ya miaka 14,400 katika makazi ya kale ya binadamu kaskazini-mashariki mwa Jordan.

 

Watafiti kutoka wamegundua kuwa binadamu wa kale walisaga, kuchuja, kukaanga na kupika nafaka pori, zikiwemo shayiri na ngano.

 

Wamesema kuoka mikate kwa nafaka pori kuliwahimiza binadamu wa kale kuanza kulima nafaka, na kuleta mapinduzi ya kilimo katika zama za mwisho za mawe.

Leave A Reply