Mike Pence Kutangaza Kugombania urais wa Marekani wiki ijayo Jimboni Iowa
Makamu wa rais wa zamani wa Marekani, Mike Pence, atazindua kampeni yake ambayo ilikuwa ikitarajiwa ya kuwania uteuzi wa chama cha Republikan kugombania urais wiki ijayo jimboni Iowa.
Kutokana na hili amekuwa mgombea mwingine katika uwanja mpana wa ugombea urais wa Republikan, na kumfanya awe mpinzani wa bosi wake wa zamani.
Pence atazindua kampeni zake mjini Des Moines Juni 7, ambayo ni tarehe yake ya kuzaliwa akifikisha miaka 64 kwa mujibu wa watu wawili wanaofahamu mipango yake ambao hawakutaka kutambuliswa.
Anatarajiwa pia kutoa video ikitoa ujumbe ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wake.
Timu yake inaona upigwaji kura wa mapema jimboni Iowa kuwa ni muhimu ili kumwezesha kupata ushindi, na washauri wanasema anapanga kufanya kampeni kwa nguvu kuwavutia wapiga kura wenye mrengo wa kidini ya kikristu ambao ni idadi kubwa ya wapiga kura wa chama cha Republikan.