The House of Favourite Newspapers

MIKE: SINA HAMU NA NDOA, IMENIKINAHI

MUIGIZAJI wa muda mrefu kwenye tasnia ya filamu Bongo, Mike Sangu amesema kuwa sio kwamba haoni wanawake wa kuoa tangu atengane na mkewe Salome Urassa ‘Thea’ bali hana hamu na ndoa tena kwani imemkinahi.

 

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Mike alisema kuwa anakutana na wanawake wengi ambao angetaka kuingia nao kwenye ndoa asingeshindwa lakini wito wa kuoa umepotea moyoni mwake.

 

“Kiukweli sina hamu ya kuoa tena mpaka moyo wangu utaka­pokubali, ni kama ndoa imeniki­nahi hivi na si kwamba sina wa kuwaoa, wapo wengi lakini bado siko tayari,” alisema Mike.

Comments are closed.