The House of Favourite Newspapers

Miliki Nyumba kwa shilingi 500 Tu

0

shinda-nyumba

WASHINDI WA DROO ZILIZOPITA

Washindi wa Droo ya Kwanza =>bit.ly/1Tq5PTu

Washindi wa Droo ya Pili ==>bit.ly/1TucKMv

Mshindi wa Pikipiki Akabidhiwa ==> bit.ly/1UmWJrf

Uzindua Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba =>bit.ly/24e5Qiv

KAMPUNI ya Global Publishers Ltd inayochapisha magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Championi, Risasi, Amani na Ijumaa Wikienda yanayosambazwa nchi nzima, imeandaa Bahati Nasibu kwa wasomaji wa magazeti yake

JINSI YA KUSHIRIKI

Msomaji atatakiwa kununua nakala moja au zaidi ya magazeti tajwa na kukata kuponi moja iliyomo ndani ya magazeti hayo. Atatakiwa kujaza jina lake kamili na anwani yake na kisha kuituma kwa njia ya posta au kuipeleka moja kwa moja katika ofisi za Global Publishers au kwa mawakala wake waliyopo sehemu mbalimbali nchini. Kwa wale wa mikoani, nao wanaweza kutuma moja kwa moja kwa mawakala wetu au kutuma kwetu kwa njia ya posta. Kutakuwa na vituo vya kukusanyia kuponi katika kila kata na mitaa mbalimbali nchini Tanzania.

ZAWADI

Bahati Nasibu hii inatarajiwa kuendeshwa kwa muda wa miezi 6, tunatarajia kutoa zawadi ya nyumba mpya mwishoni mwa mchezo huu ambayo imejengwa eneo la Salasala, Wilayani Kinondoni, jijini Dar es salaam, nyumba hiyo ni mpya kabisa na itakuwa na samani ndani na hadi sasa imeshamilika kwa alilimia 95. Pia kutakuwa na Droo nyingine ndogo kila mwezi zitakazotoa zawadi za Simu za Kisasa, Runinga na Ving’amuzi vyake, na vyombo vya mbalimbali vya nyumbani.

MASHARTI

Wasomaji wote wenye umri wa kuanzia miaka 18 wanaruhusiwa kushiriki, lakini wafanyakazi wa Global Publishers, waandishi wake na ndugu zao hawaruhusiwi kushiriki. Msomaji anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadri awezavyo ili kujiongezea nafasi ya kushinda zawadi ya Nyumba na zawadi nyingine. Kuponi zote zitaingia katika droo ndogo na kubwa.

HISTORIA YA GLOBAL KATIKA BAHATI NASIBU

GLOBAL Publishers ni kampuni pekee ya uchapishaji wa magazeti nchini ambayo imekuwa ikiandaa Bahati Nasibu na kutoa zawadi kubwa kwa wasomaji wake mara kwa mara. Imekuwa ikiendesha Bahati Nasibu mbalimbali kupitia magazeti yake tangu mwaka 2000 na kwa nyakati tofauti imeshatoa jumla ya magari 5, kama vile Nissan March, Toyota Vitz, Mitubish Pajero, Mercedes Benz na Toyota Noah na zawadi nyingine nyingi za tahamani, ikiwemo kumpeleka msoamaji wake mmoja Hong Kong kutalii.

Global Publishers imekuwa ikifanya yote haya si kwa sababu ina fedha nyingi sana, bali inafanya haya kama njia moja wapo ya kuwashukuru wasomaji wake kwa kuendelea kuyaamini na kuyasoma magazeti yake kwa zaidi ya miaka 15 sasa, pia inafanya haya kama njia moja wapo ya kurejesha kwa wasomaji sehemu ya kipato chake ili kuboresha maisha yao. Aidha inafanya hivi pia kwa ajili ya kuimarisha na kuongeza idadi ya wasomaji wake.

Mwisho, tunawahakikishia wasomaji wetu kuwa washindi wote wa Bahati Nasibu za Global publishers hupatikana kihalali chini ya usimamizi madhubuti wa Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha na huchezeshwa kwa wazi kila mtu akiona.

Tunakushukuru sana Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda kwa kuja kuizindua rasmi Bahati Nasibu hii na tunakupongeza kwa kazi yako nzuri kwa taifa.

 

Leave A Reply