The House of Favourite Newspapers

Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda kwa mtumishi wa afya

Mshindi wa zawadi ya wiki ya shilingi milioni 10 katika promosheni ya Jigiftishe na Tigo, Mbwana Saidi Mbela (wa kwanza kulia) akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi kutoka kwa Shadya Bakari (kulia) wa Tigo katika hafla iliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam. 
Mshindi wa zawadi ya wiki ya shilingi milioni 10 katika promosheni ya Jigiftishe na Tigo, Mbwana Saidi Mbela (wa tatu kulia) akipongezwa na washindi wa kila siku wa shilingi milioni moja moja.
Mmoja wa washindi wa zawadi ya kila siku ya shilingi milioni moja kwenye promosheni ya Jigiftishe na Tigo, Theresia Philipo (wa kwanza kulia) akilia kwa furaha wakati akikadihiwa  mfano wa yenye thamani ya shilingi milioni moja na Shadya Bakari (wa kwanza kushoto).
Washindi wa zawadi za kila siku za shilingi milioni moja moja katika Promosheni inayoendelea ya Jigiftishe na Tigo wakiwa na nyuso za furaha.
Mmoja ya washindi wa kila siku wa shililingi milioni moja katika promosheni ya Jigiftishe inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Khaled Miraji Sabuni (katikati) akipokea mfano wa hundi kwa wafanyakazi wa Tigo, Shadya Bakari (kushoto).

 

Mtumishi wa Wizara ya Afya kitengo cha maabara na mkazi wa  Mpwapwa mkoani Dodoma Mbwana Saidi Mbela , ameibuka mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10 za Tigo Jigiftishe  na kukabidhiwa zawadi yake  jijini Da es Salaam.

 

 

Mbela anakuwa ni mshindi wa tatu wa zawadi ya shilingi milioni 10 ambayo hutolewa kila wiki kwa mshindi mmoja kupitia Promosheni inayoendelea ya Tigo Jigiftishe. Milioni 10 ya kwanza ilichukuliwa na David Mmuni huku ya pili ikienda kwa Iyaka Seifu Muinga.

 

Mbela aliungana na washindi wengine wanne ambao ni washindi wa kila siku ambao walikabidhiwa shilingi milioni moja moja.

 

Akiongea muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake  katika hafla iliyofanyika  eneo la Chamazi jijini Dar es Salaam, Mbela alisema alipigiwa simu kuwa ameshinda akiwa likizo jijini Dar es Salaam ambapo alikuja kumtembela shangazi yake.

 

 

“Niliamua kutumia likizo yangu kuja jijini Dar es Salaam kumsalimia shangazi yangu. Nilipofika tu nyumbani kwake Chamazi, nikapigiwa simu ya kuambiwa kuwa  nimekuwa mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10,” anasema.

 

Mbela aliishukuru kampuni ya Tigo kwa zawadi hiyo na kusema kuwa atatumia fedha hizo kumalizia nyumba yake.

 

“Nawashauri watu watumie huduma za Tigo ili waweze kushinda. N rahisi sana kushinda haya mamilioni, mimi nimefanikiwa kushinda baada ya kuwa natumia huduma za tigo kama kutuma pesa, kununua muda wa maongezi, kununua umeme,” alisema.

 

Akiongea  wakati akimkabidhi mshindi huyo zawadi yake, Shadya Bakari kutoka Tigo aliwataka wateja kuendelea kutumia huduma mbali mbali za Tigo ili kujishindia mamilioni ya shilingi yaliyotengwa kwa ajili ya kuwazawadia katika msimu huu wa sikukuu.

 

Promosheni  ya Jigiftishe inayoendeshwa na kampuni ya Tigo inalenga kuwazawadia wateja wanaotumia huduma za mtandao huo katika kipindi hiki cha sikukuu na mwaka mpya.

 

Promosheni itaongeza idadi ya mamilionea katika msimu huu wa sikukuu kwa kutoa zawadi kumi za shilingi milioni moja kila siku, zawadi  moja ya shilingi milioni kumi kila wiki na zawadi kwa washindi wa jumla za shilingi milioni 15, milioni 25 na milioni 50 itakayotolewa mwisho wa promosheni.

Comments are closed.