The House of Favourite Newspapers

Milioni 200 Yanga Kimeeleweka Baada Ya Kuifunga Simba

0

IMEISHA hiyo! Ndivyo utakavyoweza kusema, baada ya Kampuni ya GSM kupanga kuwapa Sh milioni 200 wachezaji wa Yanga katika kutekeleza sehemu ya ahadi yao waliyoitoa baada ya kuwafunga watani wao wa jadi, Simba.

 

Yanga na Simba walivaana Machi 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mchezo uliomalizika kwa Simba kufungwa bao 1-0 lililofungwa na Mghana Bernard Morrison kwa njia ya faulo nje ya 18.

 

Mara baada ya mchezo huo, Yanga ilisafiri kwenda Ruangwa, Lindi kucheza na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Majaliwa ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said amezungumza na gazeti hili na kusema kuwa pesa hizo walitarajiwa kuzipata jana Jumanne baada ya taratibu za malipo kukamilika kwa wachezaji hao.

 

Said alisema kuwa lazima watimize ahadi yao, pesa waliyoitoa kwa wachezaji wao ili kuhakikisha wanatengeneza morali ya kujituma kwa wachezaji katika michezo inayofuatia ya ligi kuu ya Kombe la FA.

 

Aliongeza kuwa matokeo ya kufungwa waliyoyapata kwenye michezo miwili iliyopita walipocheza na KMC, Namungo siyo sababu ya wachezaji kucheza chini ya kiwango ni vema likafahamika hilo kwa mashabiki wa timu hiyo.

 

“Ninaweza kusema kuwa wachezaji wa Yanga ni kama tayari wamepata pesa zao zilizokuwepo katika sehemu ya ahadi yetu tuliyoitoa wadhamini GSM.

 

“Pesa hizo zilikuwa kwenye taratibu za mwisho za kukamilisha malipo yao, na kikubwa kilichochelewesha ni ratiba tuliyokuwa nayo ya kusafiri kwenda Lindi kucheza na Namungo, tuliwasubiria warejee Dar ndiyo tuwape pesa hizo.

 

“Katika sehemu hiyo ya ahadi Sh milioni 200, GSM kama wadhamini tumepanga kuwaongezea Sh milioni 10 ambayo inajulikana tunaitoa kila timu inapopata matokeo ya ushindi, hivyo itakuwepo sehemu ya mgao wa wachezaji wetu,” alisema Hersi.

Stori: Wilbert Molandi na Musa Mateja

MAGAZETI MARCH 18: KUTOKA MTAANI | WANANCHI KUHUSU CORONA | HALI ILIVYO KIMARA STAND

Leave A Reply