The House of Favourite Newspapers

Milioni 50 za Tigo Jigiftishe zaenda kwa mkulima Songea

…Sadick Zabron Kilipamwambu akifurahia ushindi.
Mshindi wa zawadi kubwa ya shilingi milioni 50 katika Promosheni iliyomalizika ya Tigo Jigiftishe Sadick Zabron Kilipamwambu (wa tatu kushoto) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja wa Tigo Kanda ya Kusini Abbas Abrahaman (wa pili kushoto).

 

 

Mkulima na mfanyabiashara wa nyanya katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Sadick Zabron, amejishindia kitita cha shilingi milioni 50 baada ya kuibuka mshindi katika droo kubwa ya promosheni iliyomalizika ya Tigo Jigiftishe.

 

Zabron ndiyo mshindi wa zawadi kubwa katika Promosheni ya Jigiftishe. Washindi wengine katika droo kubwa ni Emma Kauka mkazi wa Dar es Salaam na Abdulrazak Abdallah mkazi wa Zanzibar alijishindia Sh 15m/=

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhiwa zawadi iliyofanyika katika Soko la Manzese mjini Songea, Zabroni alisema maisha yake yatabadilika kwa kiasi kikubwa kupitia fedha hizo.

 

“Sikuwahi kuwaza kumiliki kiasi kikubwa cha fedha kama hiki, maisha yangu yatabadilika. Nitajenga nyumba nzuri na kuachana na kibanda cha nyasi nilichokuwa nikiishi na familia yangu. Naishuru Tigo kwa kubadilisha maisha yangu,” alisema.

 

 

Mshindi huyo alisema atatumia fedha hizo pia kupanua shughuli zake za kilimo cha nyanya kwa kulima mashamba makubwa zaidi na kwa kilimo cha kisasa na pia atatumia fedha hizo kuwaendeleza watoto wake kielimu.

 

Zabron alisema kushinda kwake kunatokana na kuingiza vocha za Tigo kwa ajili ya kufanya mawasiliano na wateja wake wa nyanya pamoja na kutuma au kutumiwa fedha mara kwa mara kupitia Tigo –Pesa.

 

Akizungumza wakati akimkabidi zawadi kwa mshindi, Meneja wa Tigo kwa Kanda ya Kusini Abbas Abrahaman aliwataka wakazi wa maeneo ya Songea na jirani kuendelea kutumia mtandao wa Tigo ili kuweza kunufaika.

 

“Zipo faida nyingi za kutumia Tigo. Ni mtandao wa uhakika na gharama nafuu. Leo mmeshuhudia mwenzenu akiweza kujishindia Sh milioni 50m/-kwa kutumia tu mtandao wa Tigo na hii inaonyesha kuwa Tigo inawajali wateja wake,”alisema.

 

 

Comments are closed.