Milipuko yaua watu zaidi ya 52 Uturuki
Majeruhi wakiokolewa kutoka eneo la tukio. Hali ya sintofahamu ikitanda eneo la tukio. Hali ilivyokuwa baada ya mashambulizi hayo Waliojeruhiwa wakisaidiwa na ndugu na jamaa zao.Miili ya makumi waliopoteza maisha wakati wa mashambulizi hayo.Waturuki wakikimbia kutoka eneo la tukio ili kuokoa uhai wao.
Uokoaji ukiendelea…Waliopoteza maisha. Vilio vikitawala. Kikosi maalum cha uokoaji wakiwa kaziniHali ilivyokuwa eneo la tukiuo.
Ankara, Uturuki
Milipuko miwili imetokea wakati wa mkutano wa hadhara wenye lengo la maandamano ya amani katikati mwa Mji Mkuu wa Uturuki, Ankara asubuhi ya leo na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 52 na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa vibaya.
Picha za televisheni zilionyesha watu waliokuwa na hofu na wengine wakiwa wamelala chini wakiwa wametapakaa damu miilini mwao.
Wakati duru ya pili ya uchaguzi wa ubunge ikitarajiwa kufanyika mwezi ujao, maandanmano hayo yalipangwa na vyama vya wafanyakazi wakitaka kumalizika kwa mashambulizi yanayoendeshwa na serikali dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi.