The House of Favourite Newspapers

Milipuko ya Mabomu Yaua Watu Zaidi ya Saba Indonesia

0

Jakarta-bombs

Jengo la mgahawa wa Starbucks Coffee lililopo Mji Mkuu wa Indonesia, Jakarta ambapo mabomu hayo yamelipuliwa mapema leo.

Milipuko ya mabomu takribani sita imetokea katika Mji Mkuu wa Indonesia, Jakarta na baadaye ufyatulianaji mkali wa risasi na watu zaidi ya saba wameripotiwa kuuawa japo polisi wanasema huenda kuna idadi kubwa zaidi ya waliouawa.

Kati ya hao waliouawa ni maofisa watatu wa polisi, raia wawili akiwemo Mreno mmoja pamoja na washambuliaji watano.

Jakarta-bombs (1)

Polisi wa Indonesia wakijihami

Milipuko imetokea maeneo kadha, ikiwa ni pamoja na mgahawani katika duka la kibiashara lililoko karibu na Ikulu ya rais wa nchio hiyo na ofisi za Umoja wa Mataifa (UN).

Indonesian-capital-explosions

Kuna ripoti za maafisa wa polisi kuonekana kwenye majengo na barabara za mji huo karibu na kituo hicho cha kibiashara.

Eneo hilo limezingirwa na maafisa wa usalama.

Rais Joko Widodo amehimiza raia wawe na utulivu na kushutumu “kitendo hicho cha ugaidi”.

Indonesian-capital-explosions (3)“Tunaomboleza watu waliofariki kwa sababu ya kisa hiki, lakini pia tunakilaani. Kimevuruga utulivu na amani na kuingiza wasiwasi miongoni mwa raia,” amesema.

Msemaji wa polisi, Anton Charliyan ameambia wanahabari kuwa maafisa wa polisi na raia ni miongoni mwa waliofariki.

Indonesian-capital-explosions (1)

Bado haijabainika ni nani huenda amehusika katika shambulio hilo.

Indonesia, taifa lenye Waislamu wengi zaidi duniani, imeshambuliwa na makundi ya wapiganaji wa Kiislamu awali.

Indonesian-capital-explosions (2)

Majuzi, imekuwa kwenye hali ya juu ya tahadhari kutokana na tishio kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State.

Hili ndilo shambulio la kwanza kubwa kutokea Jakarta tangu mashambulio kwenye hoteli za Marriot na Ritz mwaka 2009.

Jakarta suicide (1) Jakarta suicide (2) Jakarta suicide (3) Hali ilivyokuwa baada ya tukio hiloJakarta suicide (4) Jakarta suicide (5) Eneo ambapo moja ya bomu limelipuliwa.Jakarta suicide (6) Hali ya taharuki wakati mabomu yakiripukaJakarta suicide (7) Polisi wakifanya juhudi za kupambana na taharuki hiyoJakarta suicide (8) Jakarta suicide (9) Jakarta suicide (10) …Miili ya waliouawaJakarta suicide (11) Jakarta suicide (12) Polisi akiimarisha ulinziJakarta suicide (13) Miili ya waliouawa ikifunikwaJakarta suicide (14) Jeshi la Usalama la Indonesia wakipambana na walipuaji wa mabomu hayoJakarta suicide (15) Kikosi chaJeshi la Usalama la Indonesia wakiwa katika hekaheka ya kupambana na adha hiyo.
Jakarta suicide (17) Jakarta suicide (18)Majeruhi wakipewa msaada.Jakarta suicide (19) Jakarta suicide (20)Mmoja wa ofisa wa polisi aliyejeruhiwa kwa bomu akiokolewa.
Jakarta suicide (21) Jakarta suicide (22) Jakarta suicide (23)Anayedhaniwa kuwa mtuhumiwa akiwanyooshea bastola raiaJakarta suicide (24) Jakarta suicide (25) Jakarta suicide (26) Jakarta suicide (27) Polisi wakizidi kuimarisha ulinzi.Jakarta suicide (28) Eneo la tukio.Jakarta suicide (29) Polisi akijihami.Jakarta suicide (30)Anayedhaniwa kuwa mmoja wa watuhumiwa akikatiza na bunduki mkononi.
Jakarta suicide (31)Ofisa wa Polisi akiamurisha kikosi chake kupambana na walipuaji.Jakarta suicide (32)Mbwa wa polisi akipelekwa eneo la tukio ili kufanya utafiti wa kubaini walipuaji wa mabomu hayo.Jakarta suicide (33)

Polisi wakichukua tahadhari.

PICHA NA DAILY MAIL

Leave A Reply