The House of Favourite Newspapers

Mimba ya Jokate yazua balaa!

0

JokateNa Waandishi wetu RISASI MCHANGANYIKO

DAR ES SALAAM: Kizaazaa! Kufuatia mwanamitindo nyota Bongo na Miss Tanzania Namba 2, 2006, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ kudaiwa kuwa na ujauzito wa Mbongo Fleva, Alikiba Saleh, mazito yameibuka kwa mademu waliowahi kusemekana ni ‘zilipendwa’ wa msanii huyo kusemwa kwamba, hawakuwa na uwezo wa kumzalia, Risasi Mchanganyiko linakuwa la kwanza kukudondoshea.

jokateChanzo makini kililiambia Risasi Mchanganyiko kuwa, warembo wanaodaiwa kuwa ni wapenzi wa zamani wa Kiba ni Gift Stanford ‘Gigy Money’, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ na Sabrina Omar ‘Sabby Angel’ kwamba hawakuwa na uwezo wa kuzaa, ndiyo maana hawakuweza kushika ujauzito wa staa huyo na kuishia kuachika tu.

MSIKIE HUYU HAPA

“Wapenzi wa zamani kina Gigy Money, Sabby Angel na Amber Lulu hawakuwa na uwezo wa kuzaa ndiyo maana hawakuwahi kuonekana wakiwa na ujauzito au kusikika kwamba walikuwa na mimba ikaharibika na sasa hivi hawataki hata kusikia habari za ujauzito wa Jokate hivyo tunamsifu Jokate kama ni kweli ana mimba ya Kiba.

kiba jokateJokate na mpenzi wake, Alikiba Saleh

“Mashabiki kibao wameonekana kufurahishwa na jambo hilo kwani wamemuona ni mwanamke mwenye ujasiri licha ya kwamba Kiba ana watoto wengine watatu kwa mama tofauti, lakini yeye (Jokate) hajaona tatizo kumzalia. Inaonesha ni jinsi gani anavyompenda Kiba, kwa hiyo ni mfano wa mwanamke wa kuigwa kutokana na ujasiri na msimamo wake,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kupata ubuyu huo kutoka kwa chanzo, Risasi Mchanganyiko liliwasaka wahusika hao waliotajwa kutoka kimapenzi na Kiba ambapo kila mmoja alitoa kauli yake huku wengine wakitoa kauli za kushambulia.

BOFYA HAPA UMSIKIE GIGY MONEY

Huyu ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumza na Risasi Mchanganyiko ambaye alisema maneno makali bila kuumauma midomo kwa Kiba na Jokate pia.

“Jokate azae tu hainihusu! Ninachotafuta mimi ni pesa, maana hao watoto wapo tu muda wowote nikitaka nitazaa maana kizazi ninacho. Wanaosema sina uwezo wa kuzaa hawajawahi kunipima, Kiba amebaki kuwa X (wa zamani) wangu tu na tumewahi kufanya mengi enzi hizo wanajuaje kama niliwahi kupata ujauzito ukaharibika?”

AHOFIA MANENO MAKALI KUHARIBU MIMBA YA JOKATE

“Sitaki kumpa maneno machafu maana kama Jokate ni mjamzito mimba ikatoka bure, yeye azae naona kawaida tu hainiumizi chochote. Kwanza baba mwenyewe Kiba mwenye watoto kibao nje, wala hainisumbui. Yeye Jokate ndiye amemuona Kiba wa maana awe baba mtoto wake, he! He!

“Azae naye tu, lakini ajue atakuwa mama wa watoto wengine watatu, wa kwake atakuwa wa nne. Mimi niponipo kwanza si kama Jokate alivyoamua.”

SABBY ATOA SABABU ZA KUMBANIA MIMBA KIBA

Kwa upande wake, Sabby alifunguka; “Wanaosema sina kizazi hawanifahamu vizuri, nina mtoto mkubwa tu ambaye nilipata kwa marehemu mume wangu ndani ya ndoa na anasoma darasa la kwanza. Kiba sikuzaa naye kwa sababu sitaki kuzaa nje ya ndoa, maana nitamnyima mwanangu haki ya msingi ya kulelewa na wazazi wote wawili, pia mimi ni mtoto wa Kiislam safi.

“Sijuti maana yalikuwa ni maamuzi yangu, sizai nje ya ndoa, sitaki kumkosea Mungu, Jokate kuwa mjamzito ni jambo zuri na la heri na Kiba ni baba mzuri sana kwa sababu ana watoto watatu na kila mmoja ana mama yake, na anawahudumia ipasavyo…teh! Teh!”

AMBER LULU ACHOMOA

“Mimi siwezi kulizungumzia hilo kwa sababu sijawahi kutoka na Kiba.”

MREMBO WA KIBA ATUA BONGO

Baada ya taarifa za ujauzito wa Jokate kuzagaa, mrembo anayedaiwa kuwa ni wa Kiba, aliyetajwa kwa jina moja la Mariam, anayeishi Marekani ametua Bongo mwishoni mwa wiki iliyopita ikidaiwa ni kutaka kuhakiki kama habari za mimba ya Kidoti zina ukweli au la ili achukue maamuzi magumu!

“Jamani Mariam kaja Bongo toka Marekani, amesikia Jokate ni mjamzito, sasa amekuja kuhakikisha mwenyewe. Unajua Kiba na Mariam wamepanga mambo mengi sana, sasa anachotaka ni kujua ukweli,” kilisema chanzo chetu.

Hata hivyo, chanzo hicho kilipiga danadana kulipeleka Risasi Mchanganyiko, alikofikia mwanadada huyo kwa madai kiko bize sana.

HII NI MIMBA YA PILI

Mwaka jana, Jokate aliwahi kuripotiwa kuwa na ujauzito wa mwanamuziki huyo, lakini ukachoropoka na kusababisha penzi lao kuyumba kwa muda lakini kwa sasa anadaiwa kuwa na ujauzito tena na mapenzi yao yanasemekana yapo motomoto!

LAKINI KUNA MANENO HAYA

Hata hivyo, yapo madai mengine kwamba, Jokate si mjamzito bali anasingizia ili apate kiki kutoka kwenye familia ya Kiba ambapo inadaiwa kuwa, anaamini ujauzito unaweza kuongeza upendo kutoka kwa ndugu wa mwanamuziki huyo ambao hawamkubali.

MENEJA AMZUNGUMZIA KIBA, JOKATE

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Risasi Mchanganyiko lilizungumza na mmoja wa viongozi wa kambi ya Kiba, aliyeomba jina lake lihifadhiwe.

Kuhusu mapenzi ya Kiba na Jokate, meneja huyo alisema: “Jokate wala! Kama ni mimba mimi sijui, ila Kiba kwa sasa ana mpenzi wake, mrembo mmoja hivi, anasoma Mombasa (Kenya), lakini ni Mtanzania. Hata hivi karibuni tulipokuwa Kenya, ndiye alikuwa naye.”

KAMA NI KWELI, JOKATE KUUMWA NA DADA WA KIBA VIPI?

Licha ya tamko la kiongozi huyo, kumbukumbu muhimu kutoka kwenye makabrasha ya gazeti hili zinaonesha kuwa, kuna wakati Jokate aliumwa kiasi cha kulala kitandani, dada wa Kiba, Zabibu alimpelekea dawa na kumtakia kupona haraka (getwell soon) akiwa kama wifi yake huku bosi wake akisema; ‘wala.’

JOKATE ATAFUTWA

Ili kuleta mzani wa habari hii, juzi, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Jokate kwa njia ya simu lakini ilikuwa bize wakati wote na alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (SMS) hakujibu mpaka gazeti hili linakwenda mitamboni.

SIKU CHACHE NYUMA

Siku chache nyuma, paparazi wa Global alimtumia meseji  Jokate kumuuliza kuhusu madai ya kunasa ujauzito ambapo alijibu: Siyo kweli. Lakini hao wanaosema nina mimba wananitakia mema maana ni jambo la heri.”

KIBA NAYE

Kiba naye alipotafutwa juzi kwa njia ya simu, hakupokea licha ya kupigwa mara kadhaa, utadhani alikuwa na Jokate ‘wakaambizana’ wasipokee!!

Leave A Reply