The House of Favourite Newspapers

Mimba ya Lynn… Tanasha Yamkuta ya Zari kwa Mondi

0

MJI mzito huu! Ndiyo maneno wanayotamka watoto wa mjini kutokana na kinachoendelea kwa msanii wa muziki wa Bongo Fleva; Irene Godfrey ‘Lyyn’ mimba yake kuzua gumzo kila kona.

 

ISHU IMEANZIA INSTA

Awali, Lyyn aliweka video kwenye ukurasa wake wa Instagram ambayo ilikuwa ikimuonesha kwamba kwa sasa ana ujauzito mkubwa tu kisha baadaye kufutika licha ya kwamba wambea walikuwa wameshaichukua, hivyo kuanza kusambaa mitandaoni humo.

 

Mimba hiyo ya Lyyn ilizua gumzo la aina yake baada ya habari kueleza kuwa ni ya staa wa Bongo Fleva; Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye zamani aliwahi kuhusishwa naye kimapenzi.

TANASHA AONEWA HURUMA

Kutokana na tetesi hizo za kwamba Diamond ndiye baba kijacho, wadau mbalimbali walionekana kumuonea huruma Tanasha na kusema kuwa yale yanayomtokea yanafanana kwa kila kitu na yaliyomtokea, Zarinah Hassan ‘Zari’ ambaye ni mzazi mwenzake na Diamond.

 

“Mimba ya Lyyn ni ya Mondi na ndiyo maana hata kule Dubai wakati ameenda kufanya shoo, mwanadada huyo alihudhuria kwa sababu kuna kitu kilikuwa kikiendelea kati yao,” alisema mmoja wa marafiki wa Lyyn ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini.

 

TANASHA YAMKUTA YA ZARI

Haya yanayomtokea Tanasha kwa sasa ni kama yale yaliyotokea kwa Zari kipindi yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na Diamond. Kipindi hicho ndicho Diamond alipozaa na mwanamitindo, Hamisa Mobeto kitu kilichozua mtafaruku wa aina yake kati yake na Zari kwani alimtuhumu kwamba siyo mwaminifu ndiyo maana akachepuka na mwanamama huyo na kumpa ujauzito.

“Ni yale yale yaliyomtokea Zari, Zari alilalamika chinichini kwa muda mrefu hadi pale alipochoka akaamua kuanika hadharani. “Mondi alikuwa kila akielezwa kuhusu kuchepuka nje alikuwa anakataa, sasa baadaye Zari alichoka akaona isiwe tabu kila mtu achukue hamsini zake,” kilisema chanzo makini kilicho ndani ya familia ya Mondi.

 

Baada ya mtafaruku huo, hawakukaa muda mrefu ndipo Diamond na Zari wakaachana ambapo mpaka leo watoto wawili waliofanikiwa kuwapata wanaishi na mama yao nchini Afrika Kusini ‘Sauz’. Licha ya vyanzo mbalimbali kuihusisha mimba ya Lyyn na Diamond, staa huyo wa Bongo Fleva hajakanusha wala kukubali popote na alipotafutwa na gazeti hili, simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

 

LYYN ACHEEKA

Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Lyyn kwa njia ya simu ili kueleza ukweli wa nani baba kijacho wake ambapo mazungumzo yalikuwa hivi;

Risasi: Hongera kwa kuwa mama kijacho.

Lyyn: Asante sana.

Risasi: Kuna tetesi kwamba baba mtoto wako mtarajiwa ni Diamond, hili likoje?

Lyyn: Anaangua kicheko (hahahaha), naomba nicheki baadaye tutazungumza kuhusu hilo. Alipopigiwa tena baada ya muda, Lyyn hakupokea tena simu.

TANASHA ANASEMAJE?

Ili kuujua ukweli, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Tanasha lakini hakupatikana ila ikumbukwe kuwa hivi karibuni mwanamama huyu aliibuka na kueleza kuwa hamtegemei Diamond, bali maisha yake anayaendesha kwa nguvu zake mwenyewe.

Tanasha ni mrembo ambaye wazazi wake wana asili mbili; Mkenya na Mwitaliano, pia amekuwa mwanamitindo kwa kipindi kirefu.

 

TUJIKUMBUSHE

Diamond aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na Tanasha mwishoni mwa mwaka juzi ikiwa ni baada ya kumwagana na Zari ndani ya mwaka huohuo siku ya Wapendanao yaani Februari 14, 2018

STORI: WAANDISHI WETU, RISASI

Leave A Reply