The House of Favourite Newspapers

MIMBA YA ‘MATAMBARA’ YAMUUMBUA HUSNA

MIMBA YA 'MATAMBARA' YAMUUMBUA HUSNA
Husna Maulid.

MIMBA ya Husna Maulid ilikuwa ya  kughushi.  Imemuumbua baada ya kugundulika kuwa hakuwa nayo, badala yake alikuwa akiweka matambara tumboni kuonesha ana mimba. Kwa  mujibu chanzo makini, Husna hakuwa na mimba, lakini alikuwa akiweka matambara hayo kwa ‘utashi’ wake ili aonekane tu ana ujauzito lakini hakuwahi kuwa nayo.

“Nilikuwa  na MIMBA ya kughushi aliyokuwa akiiweka Video Queen wa Bongo, Husna Maulid imemuumbua baada ya kugundulika kuwa hakuwa nayo, badala yake alikuwa akiweka matambara tumboni kuonesha ana mimba.

ninashangaa sana kwa nini Husna, alikuwa akiweka matambara ili aonekane ana mimba kitu ambacho wengi waliamini hivyo,” kilisema chanzo. Gazeti hili lilimtafuta Husna ili kuzungumzia ishu hiyo ambapo badala ya Husna kujibu hoja, aliangua kicheko na kusema yote ni ya walimwengu. “Daah sijui nizungumzeje hiyo ishu maana yote ni ya walimwengu bwana wee yaache si unajua tena mjini hapa,” alisema Husna.

STORI: IMELDA MTEMA| AMANI

Chadema Watangaza Maandamano, Wataka Lissu Aachiwe Ngeleja Akamatwe

Comments are closed.