The House of Favourite Newspapers

MIMBA YA SARAH WA HARMONIZE ILIVYOYEYUKA

MSHTUKO! Ile mimba iliyokuwa inawanyima usingizi wengi ya mchumba wa msanii wa Bongo Fleva anayeitumikia Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ aitwaye Sarah imeyeyuka, Ijumaa Wikienda limemshuhudia akiwa ‘flati’.  

 

Mwishoni mwa wiki iliyopita Sarah aliibuka kwenye bethidei ya staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper iliyofanyika kwenye Ukumbi wa New Life uliopo Mwenge jijini Dar akiwa hana ujauzito, jambo lililozua minong’ono mingi.

 

Tukio hilo lilijiri ikiwa ni mwezi uliopita tu ambapo Sarah alitupia picha zilizomuonesha ni wa kujifungua muda wowote. Kabla ya kutupia picha hiyo kulikuwa na madai na minong’ono mingi kuwa mchumba huyo wa Harmonize alikuwa haonekani mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa huko nyuma kwa sababu eti alikuwa analea mimba hiyo hivyo hakutaka kujitokeza hadharani.

“Jamani huyu ni Sarah ambaye alikuwa mjamzito? Si alikuwa na mimba kubwa tu? Sasa mbona hamna kitu kabisa au mimba imechoropoka maana kila wakati tunasikia ana mimba alafu hatuioni tena?” Alisikika mmoja wa wahudhuriaji wa shughuli hiyo ya Wolper.

 

Baada ya kuwepo kwa ubuyu huo ulioonekana kuwashangaza wengi, Ijumaa Wikienda lilimfuata Harmonize ambaye naye alikuwepo ukumbini hapo na kumuuliza kuhusu hilo.

Katika majibu yake, Harmonize aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, kama watu wanavyomuona Sarah hana hiyo mimba ndivyo ilivyo na mambo mengine ni ya kifamilia zaidi hivyo hawezi kuyaweka hadharani kila mtu akafahamu.

 

“Sidhani kama kila kitu ni vizuri kukiweka kwenye hadhara. Ni jambo kubwa hilo, lakini ni la kifamilia zaidi,” alisema Harmonize na alipoulizwa kama Sarah alikuwa amejifungua alisema: “Kama anavyoonekana, hajajifungua na hana mimba kweli.” Mara kadhaa Sarah amekuwa akidaiwa kuwa mjamzito, lakini tetesi hizo huyeyuka kama ilivyoyeyuka mimba hiyo.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Comments are closed.