Mimba Yampeleka Puta Queen Darleen

MIMBA ya msanii wa Bongo Fleva, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’, inadaiwa kumpeleka puta, IJUMAA WIKIENDA limedokezwa.

Queen Darleen ni first lady wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) inayomilikiwa na kaka yake, mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

 

Jumbe anazoweka kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii (Instagram), ndizo zimeibua madai hayo ya kupelekwa puta na ujauzito aliobeba wa mumewe ambaye ni mfanyabiashara maarufu jijini Dar aitwaye Isihaka Mtoro.

Mwanamama huyo anadaiwa kutumia kurasa zake hizo kumpiga vijembe mke mwenzake aitwaye Sabra.

 

Mabango hayo yanadaiwa kumlenga Sabra ambaye ni mke mkubwa wa mwanaume huyo, Isihaka.

Awali, wanawake hao; Queen Darleen na Sabra, walidaiwa kubeba ujauzito kwa mpigo (dabodabo) na kugeuka gumzo mitandaoni.

 

Hata hivyo, kwa bahati mbaya, ilisemekana kwamba ujauzito wa Sabra uliharibika ukiwa na miezi miwili.

Ilidaiwa kuwa, kitendo hicho kilimfanya Queen Darleen kujimwambafai kuwa ndiye wa kumzalia Isihaka ambaye alisaka mtoto kwa muda kutoka kwa Sabra bila mafanikio.

 

Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na Queen Darleen, staa huyo amekuwa akimsimanga mwenzake bila kujua kwamba hata wa kwake unaweza kuharibika.

Katika moja ya posti zake, Queen Darleen aliweka ujumbe uliodaiwa kumlenga mwenzake kuwa hana uwezo wa kuzaa.

 

Aliandika; “Jamani kuna tamthiliya inaitwa Rubyring, mnaijua? Acheni bana, kumbe vipo katika maisha hayahaya tunayoishi. Sasa itakusaidia nini kujizulia; wakati unajijua uwezo wa kubeba mii…hunaa weee tulia tu…”

Baadaye aliweka ujumbe mwingine; “Tafuta kwanza dawa ya ukurutu na sugu kisha ucheze na watoto wenzako na si mimi hapa…”

 

Kwa mujibu wa wafuasi wake, mambo hayo anayoyafanya, yanachochewa na homoni wanazokuwa nazo wanawake wanapokuwa wajawazito.

Alipotafutwa na gazeti hili, Queen Darleen alikanusha kumlenga mtu.

STORI: MEMORISE RICHARD, DAR

Toa comment