The House of Favourite Newspapers

MIMI MARS AMFUNGUKIA RAMMY

BAADA ya mkali wa filamu Bongo, Rammy Gallis kuibuka na kusema kuwa anatamani kuonana naye ikiwezekana kuanzisha naye uhusiano, msanii wa Bongo Fleva, Mimi Mars amefungukia msanii huyo kuwa hamjui vizuri na aliwahi kumuona mara moja tu ambayo ni kwenye msiba wa video vixen, Agnes Masogange.  

Akizung-umza na Showbiz Xtra, Mimi Mars ambaye pia ni mdogo wa mkali wa Bongo Fleva, Vee Money alisema kwamba hajawahi kumtaja Rammy katika mahojiano yoyote kama anavyodai msanii huyo. “Jamani hapana yule kaka nimemuona mara moja tu kwenye msiba wa Masogange alipozimia akiwa ameshika kitambaa na si vinginevyo kabisa, sijawahi wala kutamka sehemu kuwa nampenda au nataka kuonana naye,” alisema Mimi Mars.

Kwenye mahojiano ya gazeti dada la hili la Ijumaa, Rammy alisema anampenda sana Mimi na kudai kuwa anajua hata yeye anampenda kwani alishawahi kumsifia alipokuwa akihojiwa redio moja

Comments are closed.