The House of Favourite Newspapers

MIMI MARS ANANGWA KURUDIA NGUO

Marianne Mdee ‘Mimi Mars’

MSANII wa Bongo Fleva, Marianne Mdee ‘Mimi Mars’ amejikuta akinangwa vilivyo na mashabiki baada ya kurudia nguo alipokuwa kwenye mahojiano na runinga moja nchini.  

Mimi Mars alionekana akiwa amevaa gauni pamoja na nywele hizohizo mwezi wa kwanza mwaka huu, alipokuwa kwenye uzinduzi wa albamu ya dada yake iliyojulikana kwa jina la Money Mondays na juzikati akarudia tena kwenye mahojiano hali iliyosababisha watu kumshambulia kwamba inakuwaje anarudia mavazi wakati yeye ni staa.

 

Risasi Vibes lilimtafuta Mimi Mars na kumuuliza kuhusiana na kunangwa huko ambapo alisema haoni tatizo kurudia nguo. “Binafsi sioni tatizo kurudia nguo ila watu wanaongea kwa sababu mimi ni staa, niwaombe tu mashabiki zangu tufuatiliane kwenye kazi na siyo mambo yasiyokuwa na maana,” alisema Mimi Mars.

Stori: MEMORISE RICHARD

Comments are closed.