The House of Favourite Newspapers

Mimi na Mungu Wangu; mtihani mgumu wenye mafunzo lukuki!

0

wanafunzi1SITAKI kuwa na maneno mengi juu ya kazi hii. Miongoni mwa kazi ambazo kamwe haziwezi kufutika akilini mwangu ni pamoja na filamu ya Mimi na Mungu Wangu. Hakika hii ni filamu ambayo imeakisi maisha halisi ya tamaduni za Kiafrika.

Mkasa wa filamu hii, unaangazia maisha ya familia ambayo inaongozwa kwa misingi na maadili bora sana yenye watoto wawili, Tino na Esha Buheti ambao wanaishi maisha ya kuchukiana kulikopindukia.

Mwanzoni, familia hii iliishi maisha ya furaha ambapo baba na mama wakiwa hai lakini mambo yanaanza kuwa magumu baada ya kufariki kwa baba wa familia (Mzee Kambi) na kubaki na mama (Hidaya Njaidi) kama mlezi na kiongozi mkuu wa familia. Tino, akiwa mwanafunzi anajikuta akisitisha masomo baada ya kushindwa kumudu gharama ikiwemo ada na michango muhimu ya shule.

Mbaya zaidi, Tino anafukuzwa kwenye chumba cha mtihani kutokana na madeni mengi ikiwemo kutolipia mtihani. Ni siku hiyohiyo ndiyo anampoteza mama yake mzazi baada ya kuugua muda mrefu. Mtihani wa maisha unaanzia hapo, kwani Tino anabaki na dada yake tu, yeye akiwa kama nguzo kuu.

Kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha, anaanza kubangaiza kwa kufanya vibarua mbalimbali, hadi alipokutana na rafiki yake wa siku nyingi akiwa mwenye mafanikio makubwa na kumdadisi siri ya mafanikio yake, ambaye anamwambia ukweli na kumpeleka kwa mganga ili naye atajirike.

Ni huko ndiko anakutana na sharti la kutembea na dada yake, jambo ambalo linaonekana gumu kwake, japo baadaye alilitekeleza na kusababisha dada yake kushika mimba ambayo analazimika kuitoa kwa shinikizo la Tino.

UHALISIA

Kwanza ni aina ya maisha ambayo Tino aliishi na dada yake ya kutopendana. Ni maisha ambayo yanatafsiri ukweli halisi, kwani mara nyingi sana watu wanaofuatana kuzaliwa hususan wakiwa wa jinsia tofauti, upendo huwa mdogo sana, kawaida huishi kwa chuki.

Esha Buheti anaibeba zaidi filamu hiyo kwa kuvaa uhalisia wa ukorofi uliopindukia, akipingana na kaka yake aliyekuwa akimchunga kupitiliza na kumzuia kuolewa na mwanaume aliyempenda. Tino anaanzisha vita nzito na Musa, kijana mstaarabu aliyempenda na kutaka kumuoa Esha.

Uhalisia mwingine unaonekana wakati Tino akimfukuza kwa panga Musa, ni tukio ambalo kwa macho ya kawaida halionekani kama igizo, alivaa uhalisia kwa kiwango kilichoendana na ukweli wa mazingira.

Kipande kingine kilichobeba uhalisia, ni wakati Tino anakutana na Musa akitoka kuswali na kumpiga mkwara mzito wa kuachana na dada yake, hapa ndipo walidhihirisha kiwango cha uigizaji kwani walionekana kuwa ‘siriaz’ na wanachokifanya.

Yapo maeneo mengi yaliyoibeba filamu hii katika suala la uhalisia. Mfano mwingine ni siku ambayo Tino akiwa mwanafunzi anadondosha pesa na kupanda daladala ambapo kondakta alipomdai pesa anajikuta hana, hakika Tino alionesha kipaji cha uigizaji kwani iliakisi uhalisia wa mtu aliyepoteza pesa bila kujua.

Miongoni mwa kosa la msingi ambalo liko wazi, ni lile la Esha Buheti kupandisha sauti kila wakati akiwa na kaka yake Tino hata katika mazungumzo ya kawaida. Kwa kitaalam hali hiyo huitwa Over acting (kuvuka mipaka ya uigizaji).

dkt. magufuli mwanzo mzuri, naamini si nguvu ya soda!

KWAKO Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Habari yako mkuu? Habari ya hapo ikulu? Bila shaka umeanza kupazoea sasa, si mgeni sana kwani kesho utakuwa unafikisha wiki.

Ukitaka kujua afya yangu, mimi ni mzima. Namshukuru Mungu naendelea kuchapa kazi katika eneo langu. Nitumie pia nafasi hii kukupongeza kwa ushindi ulioupata. Natambua changamoto kubwa uliyoipata kutoka kwa wapinzani lakini kama ulivyosema siku unaapishwa; wewe ndiyo rais na makamu wako ni mama Samia Suluhu Hassan.

Dhumuni la kukuandikia barua hii ni kutaka kukueleza kwamba usikubali kukatishwa tamaa. Wapo watu wachache ambao kwa hulka wanazozijua wenyewe, wasiopenda kuona unafanya kazi, wanakuchukia na kueneza uzushi mitaani.

Watu wa aina hiyo hawakubaliani na kasi yako. Hawafurahishwi. Asili ya watu hao ni uvivu. Wakiona mtu anafanya kazi sana, wanasema anapenda sifa. Wengine wanasema eti ni nguvu ya soda, wapuuze. Kwanza wanaosema wewe kufanya ziara kama ile uliyofanya wiki iliyopita pale Wizara ya Fedha ni nguvu ya soda, wanadhihirisha kwamba hawakujui.

Watakuwa wamekufahamu baada ya wewe kuwa rais. Wamekariri kwamba kila kiongozi anayetoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni mchafu. Wanafikiri na wewe unaishi katika mfumo wa watu wabaya wa CCM, wanajiongopea. Mimi nakufahamu wewe kupitia utendaji wako.

Sina shaka hata kidogo na uchapakazi wako. Nilipoona umeshtukiza Wizara ya Fedha, sikushangaa. Ninajua ndiyo kawaida yako. Umeshafanya mara chungu nzima wakati ulipokuwa Waziri wa Ujenzi. Ulifanya hivyo kwa wasimamizi wa mizani, ulifanya hivyo kwa makandarasi wa barabara, achilia mbali wale wajenzi wa majengo ya serikali.

Ulifanya vile ukiwa waziri sasa ni rais, nini kitakushinda? Kwangu mimi wewe naona ni zaidi ya rais. Umeletwa kuwatumikia Watanzania. Fanya kazi baba, usisikilize majungu. Nchi yetu ipo hapa ilipo kwa sababu kuna ‘majambazi’ wengi wanafanya ‘madudu’ yao kwa kujificha.

Kuna hila za kila namna katika huduma zetu za kila siku. Ukienda mahospitalini watendaji wanawanyanyasa wagonjwa. Wanafanya kazi utafikiri wamelazimishwa, madawa hakuna lakini kwenye maduka ya madaktari yanapatikana.

Watumishi wa serikali wanafanya kazi kwa masaa mawili matatu wanarudi nyumbani. Kutwa nzima wanashinda Facebook, kusoma magazeti na kupiga stori zilizojiri wakiwa katika mapumziko ya wikiendi.

 Wanasahau kwamba kutofanya kwao kazi kwa ufanisi ndiyo matokeo ya nchi kutopiga hatua.

Maisha magumu halafu wanajifanya kumuangushia lawama rais. Usikubali, wakomeshe watendaji wazembe waliozoea kuishi kwa mazoea. Watimue kazini ili na wao wayaone machungu ya kutokuwa na kazi.

Namuomba Mungu azidi kukujalia utashi, hekima na busara zaidi uweze kufanya maamuzi sahihi na yenye tija kwa taifa, Mungu akusimamie.

Ni mimi ndugu yako;

Erick Evarist

Leave A Reply