The House of Favourite Newspapers

Mipango ya Mbelgiji Atakavyowaingia Waarabu

KOCHA wa Simba, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji, ameweka wazi kuwa licha ya kutumia mechi za SportPesa kama sehemu ya kujiandaa na mechi yao dhidi ya Waarabu, Al Ahly, ataingia kwenye mechi hiyo na umakini wa hali ya juu.

 

Simba wanatarajia kushuka dimbani Februari 2, kuvaana na Al Ahly katika mechi ya tatu ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba hadi sasa wameshacheza mechi mbili za hatua hiyo na JS Saoura waliyoshinda 3-0, pia AS Vita waliyofungwa 5-0.

Kocha huyo ameliambia Championi Jumatatu, kuwa anajua ugumu wa mechi hiyo na Al Ahly jambo ambalo linamsababisha yeye na kikosi chake kuingia kwa umakini wa hali ya juu.

 

“Tulikuwa na muda mzuri wa kujiandaa kutokana na michuano ya SportPesa ambapo tulicheza na timu za Kenya. Hayo yalikuwa mazoezi tosha kwetu.

“Lakini hata hivyo tunaelewa juu ya ugumu wa mechi hiyo ambayo itakuwa ugenini kiasi kwamba inatufanya tuingie uwanjani tukiwa na umakini wa hali ya juu sana,” alisema kocha huyo.

MARTHA MBOMA NA SAID ALLY.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.