Miquissone Aondolewa Simba

MENEJA wa klabu ya Simba, Abbas Ally, amesema kuwa kiungo wa timu hiyo, Luis Miquissone, ameondolewa kikosini na kuwekwa chini ya uangalizi wa madaktari kutokana na kupata maumivu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya FC Platinum uliochezwa wiki iliyopita kwa Mkapa.

 

Abbas alisema Miquissone hakusafiri kwenda Zanzibar na wenzake baada ya kufanyiwa vipimo na madaktari wakamkata abakie Dar ili aweze kupewa matibabu na muda kidogo wa kupumzika na kisha mwili wake ukiwa sawa ndipo ajiunge na timu.

 

“Kweli Miquissone amebakia Dar akipatiwa matibabu baada ya kupata ‘injuries’ kwenye mchezo uliopita dhidi ya Platinum. Hivyo akirejea katika hali yake ya kawaida atajiunga na timu,” alisema Abbas.

 

Simba wametinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi na watakutana na Namungo leo Jumatatu

Stori: ISSA LIPONDADar es Salaam

Toa comment