The House of Favourite Newspapers

OFM Yanasa Misosi Ikiuzwa Kiholela Dar

1

OFM Chakula (5)Mishikaki na ndizi za kuchoma vikiuzwa kihohela

Deogratius Mongela na Mayasa Mariwata

LICHA ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Ummy Mwalimu (pichani juu) kukemea uuzwaji holela wa vyakula na matunda kuepuka ugonjwa wa kipindupindu, OFM imebaini bado uuzwaji wa bidhaa hizo umeshamiri jijini Dar.

OFM Chakula (2)
Waziri huyo alitoa hadhari ya ugonjwa huo, Desemba 16 , mwaka jana ambapo Desemba 28, alizidi kutilia mkazo kwa kuwataka wananchi wajiepushe na vitendo mbalimbali vinavyosababisha ugonjwa huo ikiwemo kula chakula bila kunawa mikono, ulaji wa vyakula hovyo na kula matunda ambayo yamekatwa barabarani.

OFM Chakula (6)Hali halisi ya uuzaji vyakula holela ilivyo katika baadhi ya maeneo jijini Dar.

Mapema wiki hii, waandishi wetu wa Kitengo Maalum cha Kufichua Maovu (OFM) walipita maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar yakiwemo Buguruni-Sheli, Malapa, Urafiki-Njia Panda ya Mabibo na Kariakoo-Big Bon na kujionea vyakula kama ndizi, mishikaki na matunda mbalimbali vikiendelea kuuzwa kiholela.

OFM Chakula (8)Akizungumzia uuzwaji huo, mmoja wa wakazi wa Kariakoo aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema wanaoendelea kununua na kuuza vyakula hivyo wote wanafanya makosa hivyo ni vyema serikali ikawachukulia hatua zaidi.

OFM Chakula (9)“Haiwezekani mtu unaambiwa kuna kipindupindu, unaona kabisa wagonjwa wanaongezeka kila siku halafu wewe unathubutu kula hovyo, hawa wanaouza nao wanapaswa kuchukuliwa hatua,” alisema mkazi huyo wa Kariakoo.

OFM Chakula (4)OFM ilibaini wauzaji wengi wa vyakula kama mishikaki na ndizi za kuchoma wanatii agizo la serikali lakini ikifika muda wa jioni wanakaidi kwa kuuza kinyemela pasipo kujua wanahatarisha afya za watu.

OFM Chakula (3)OFM ilimtafuta Waziri Ummy ili azungumzie ukiukwaji wa agizo lake lakini bahati mbaya simu yake haikuwa ikipatikana hewani hadi tunakwenda mitamboni.

1 Comment
  1. Abby says

    Hii ni hatari kiafya!

Leave A Reply