The House of Favourite Newspapers

Miss Dunia Kiziwi Atikisa Bongo

IMEZOELEKA kuwa warembo wengi wanapotwaa taji la umiss hata la mkoa ni vigumu kumkuta akijichanganya kwenye daladala, bajaj au hata bodaboda.

 

Kwa mrembo aliyetwaa taji la Top Model katika mashindano ya Miss Dunia upande wa walemavu wa kusikia ‘viziwi’, Winfrida Bryson, ni tofauti baada ya Jumamosi iliyopita kunaswa akiwa anakwea bajaj maeneo ya Posta jijini Dar.

 

Miss huyo alikuwa na njemba wawili ambao walionekana kuwa ni wapambe wake ambapo akiwa sambamba nao walikwenda kupatana bei na bajaj na kuzua mjadala ambao baadhi ya watu walijiuliza imekuwaje mrembo huyo kupanda bajaj?

 

“Inakuwaje mshindi na mrembo kama huyu ambaye amefanikiwa kuliwakilisha vyema Taifa ahangaike kwa usafiri wa bajaj za kukamata barabarani wakati imezoeleka kuwa wanapewa zawadi kama magari kwani huyu hajapewa?” alihoji mmoja wa watu.

 

Hata hivyo, baada ya tukio hilo mwandishi wetu aliwasiliana na mrembo huyo ili kujua kiasi cha mkwanja aliokabidhiwa kwenye michuano hiyo ambapo alisema hawakupewa fedha taslimu zaidi ya tuzo tu.

 

“Baada ya kuibuka mshindi nilichokabidhiwa ni tuzo tu sijapewa fedha,” alisema mrembo huyo.

Kuhusu kukwea bajaj mrembo huyo alisema hiyo ni kawaida kwake na hawezi kubadilika kwa sababu ya kushinda taji la Miss Dunia kipengele cha Top Model.

Stori: Richard Bukos na Neema Adrian

 

 

Comments are closed.