The House of Favourite Newspapers

Miss Kinondoni 2019 Watambulisha Zawadi ya Gari

Washiriki wa Miss Kinondoni 2019 wakiwa mbele za gari litakalotolewa kwa mshindi.

MISS KINONDONI 2019 imezinduliwa rasmi leo Juni 29, 2019 ndani ya Viwanja vya The Life Club (Maisha Club), Mwenge jijini Dar ambapo warembo 18 wameshiriki kuosha magari ambapo pesa iliyopatikana inatarajiwa kwenda kwenye kituo cha watoto yatima cha Malaika, pia wakatambulisha gari aina ya Mini Cooper (nyekundu) ambayo itakabidhiwa kwa mrembo atakayeibuka kidedea.

Akizungumza na mtandao huu, mratibu wa shindano hilo, Nancy Joseph kutoka Super Model alisema wamejipanga kikamilifu kuhakikisha na mwaka huu mshindi wa Miss Tanzania anatokea Kinondoni.

“Mwaka jana mshindi wa Miss Tanzania, Queen Elizabeth alitokea Kinondoni kwa hiyo tuna imani na mwaka huu atatokea huku huku, tuna imani hiyo,”alisema Nancy.

Naye Andrew Carlos ambaye ni mwakilishi kutoka Global Publishers ambao ni kati ya wadhamini wa shindano hilo alisema siku ya kilele, Julai 13, mwaka huu litaruka mubashara kupitia Global TV Online.

Mratibu wa shindano hilo, Nancy Joseph ‘Supermodel’ akiongea jambo kabla ya zoezi la kuosha magari kuanza.

“Tumekuwa na ushirikiano na Miss Kinondoni mara nyingi na kama Global Publishers tunatoa ahadi ya kulirusha live na pia litasikika kupitia +255 Global Radio.


“Pia Global Publishers ambao ni watayarishaji na wachapishaji wa Magazeti ya Championi, Spoti Xtra, Risasi, Amani, Ijumaa na Uwazi tunatoa ahadi kwa mshindi wa kwanza hadi tano kuwafanyia coverage baada ya shindano,”alisema Carlos. 

Comments are closed.