Miss Tanzania 2016 Arejea Nyumbani, Aahidi Kuanika Figisu Alizofanyiwa na Miss Kenya

miss-tanzania-diana-3Miss Tanzania 2016, Diana Edward Lukumay alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

miss-tanzania-diana-4Akiwa na mama yake mzazi.

miss-tanzania-diana-5

miss-tanzania-diana-6…Akisaidiwa mizigo.

miss-tanzania-diana-7

Na:Mayasa Mariwata na Gabriel Ng’osha/GPL

DAR ES SALAAM: Miss Tanzania 2016, Diana Edward Lukumay, leo Desemba 21, 2016 amerejea nchini akitokea Oxon Hill, Maryland nchini Marekani, alikoenda kuiwakilisha Tanzania katika mashindano makubwa ya urembo, Miss World 2016.

miss-tanzania-diana-10…Akiwaagamashabiki walifika kumpokea.

Akizungumza na Global TV Online baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Diana aliwashukuru sana Watanzania kwa kumpigia kura na kila aina ya ushirikiano waliouonesha ingawa hakuweza kufanikiwa kurudi na ushindi kwa kile kinachoonekana kuwa kuna figisufigisu nyuma ya pazia alizofanyiwa na Miss Kenya 2016.

miss-tanzania-diana-9…Akiingia ndani ya gari kwa safari ya kuelekea nyumbani.

“Niwashukuru Watanzania wote kwa kunipa ushirikiano wa kunipigia kura na vitu vingine, ingawa sijarudi na ushindi ila nimejifunza kumbe Mwafrika mwenzako ndiye haswa anaweza kukumaliza, nadhani tukikamilisha vielelezo vyote kila kitu kitakuwa wazi kilichotokea kwangu na Miss Kenya,” alisema Diana.

miss-tanzania-diana-1…Akizungumza na wanahabari

Mashindano hayo yaliyofanyikia kwenye Ukumbi wa MGM National Harbor, Jumapili iliyopita, Miss Puerto Rico, Stephanie Del Valle aliibuka kidedea huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Miss Dominican Republic, Yaritza Miguelina Reyes Ramirez huku Miss Indonesia, Natasha Mannuela akishika nafasi ya tatu. Mkenya Evelyn alishika nafasi ya tano.


Loading...

Toa comment