Miss Tanzania 2017 Anusurika Kutekwa

Diana Edward

DAR ES SALAAM: Mrembo anayeshikilia Taji la Miss Tanzania 2016/17, Diana Edward amenusurika kukeketwa na ndugu zake nyumbani kwao, Sakina jijini Arusha.

 

Akizungumza na Ijumaa mapema wiki hii akiwa katika mazungumzo na warembo waliokuwa wakishiriki kinyang’anyiro cha kumsaka Miss Ubungo 2017 yaliyofanyika Ukumbi wa JBN, Kijitonyama jijini Dar, Diana ambaye kiasili ni Mmasai alisema kuwa, tukio hilo hatalisahau kwa kuwa alifanikiwa kuchoropoka mikononi mwa ndugu zake hao waliotaka kuhakikisha anafanyiwa tohara hiyo kama wenzake. “Kwa mila za kwetu mwanamke ukifikia umri fulani ni lazima afanyiwe ukeketaji.

 

Kwangu mimi sikutaka kabisa kitu kama hicho kinitokee lakini kitendo cha kutia mguu nyumbani kwetu hivi karibuni huko Sakina, ndugu pamoja na watu wengine walinifuata na kunitaka nikeketwe, kisa kutimiza mila.

 

“Hata hivyo, nilifanikiwa kutoka mikononi mwao japokuwa hadi sasa hivi bado kuna ndugu wanaendelea kushikilia msimamo wa mimi kufanyiwa hivyo, lakini mwisho wa yote sikukubali kufanyiwa mambo yaliyopitwa na wakati,” alisema Diana huku akilengwa na machozi. Diana alikuwa Miss Tanzania mwaka jana katika kinyang’anyiro kilichofanyika jijini Mwanza akiwakilisha Wilaya ya Kinondoni.

Stori: Richard Bukos

Niyonzima Aeleza Kwanini Bado Ana Jezi za Yanga Amezihifadhi

Toa comment